Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira  ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Jackson Kiswaga (Mb) imewasili Mkoani Manyara Leo tarehe 17 Machi, 2023 kwa ziara ya ukaguzi wa  miradi  na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mheshimiwa Makongoro Nyerere.

Wakiwa Mkoani Manyara Kamati ya Maji na Mazigira wamekagua hatua iliyofikiwa kwenye mradi wa Maji katika Wilaya ya Babati. Mradi huo uliopo Singu na utakao hudumia maeneo ya Dareda - Singu - Sigino unaotekelezwa na BAWASA.

Akiongea mara baada ya kukagua mradi huo Mwenyekiti alisema ana mshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa na utayari wake wa  kutoa fedha nyingi kwenye miradi ya Maji nchini. 

Katika hatua nyingine Mwenyekiti ameishukuru Wizara ya Maji chini ya Waziri Juma Aweso (Mb) akisaidiwa na Naibu Waziri Maryprisca Mahundi (Mb) na Katibu Mkuu Kemikemba na wataalam wote kwa kazi kubwa wanayoifanya na utayari wa kuhakikisha watanzania wanaendelea kuneemeka na huduma ya maji. 

Kikubwa ni kuendelea waamini na kuwatumia wataalamu wa ndani  wenye uwezo wa kubuni miradi na kuitekeleza tena kwa gharama nafuu kwani mradi huu kwa awali mkandarasi wa nje angekamilisha kwa kiasi cha Bilioni 27 lakini sasa unaenda kutekelezwa na mkandarasi wa ndani kwa kiasi cha Bilioni 12.













Share To:

Post A Comment: