Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka miwili tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani. Kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita na kulia ni Katibu Tawala Msaidizi eneo la Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKOA  wa Singida kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tangu awe madarakani kuanzia 2021/2022 na 2022/2023  bajeti ya Sekretarieti ya mkoa na Halmashauri imeongezeka kutoka Sh.180,187,060,500 mwaka 2020/2021 hadi Sh.239,808,9771,000 mwaka 2022/2023.

Hayo yameelezwa leo Machi 18, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka miwili tangu Rais Samia  aingie madarakani.

"Ongezeko hili la bajeti limesaidia sana kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi katika mkoa wetu wa Singida" alisema Serukamba.

Alisema mafanikio hayo ya Serikali ya awamu ya sita ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 20220-2025 na yanapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo hapa nchini.

Serukamba alisema katika kipindi hicho cha miaka miwili bajeti ya mapato ya ndani ya Halmashauri imeongezeka kutoka Sh.16,898,296,912 mwaka 2020/ 2021 hadi kufikia Sh. 22,441,480,865 mwaka 2022/2023.

Aidha, Serukamba aliongeza kuwa  Serikali Kuu imeidhinisha bajeti ya Sh.1,053,240,000 kwa mwaka 2022/ 2023 kwa ajili ya kuwalipa madiwaniposho, posho za madaraka kwa watendaji wa vijiji posho za kila mwezi badala ya fedha hizo kulipwa na halmashauri.

Alisema mpango huo wa Serikali Kuu wa kuwalipa madiwani na watendaji wa kata na vijiji posho hizo haujawahi kufanyika katika awamu zote za Serikali zilizopita jambo ambalo limewapa ari ya kufanya kazi kwa bidii watendaji hao.

Akiongelea mafanikio hayo Serukamba alisema mkoa ulipokea Sh.2,850,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala katika halmashauri ya Wilaya ya Singida, Singida Manispaa na Ikungi pamoja na ujenzi wa nyumba za Wakurugenzi katika Halmashauri za Iramba, Singida na Mkalama.

Serukamba alielezea mafanikio hayo katika sekta mbalimbali zikiwemo za Afya, Elimu, Uzalishaji, Upatikanaji wa huduma za maji, sekta ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, ujenzi wa barabara, ujenzi wa madaraja na Sekta ya Nishati na Madini alisema Serikali imetoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Serukamba alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dk. Samia  kwa mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka miwili tangu aingie madarakani na amewaomba watanzania waendelee kumuombea na kuwa Mungu ampe afya na maisha marefu.

Viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo wa kupokea taarifa hiyo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita, akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akitoa taarifa ya mafanikio ya wilaya hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, akinogesha mkutano huo kwa wimbo wa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa katika nchi tangu aingie madarakani.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro Issa akizungumzakatika mkutano huo kabla ya kumuombea dua Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwaambayo nchi imeyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu aingie madarakani.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati  Dkt. Sprian Hilint akizungumza katika mkutano huo.
Taswira ya mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Editha Majura, Claudia Kayombo na Thobias Mwanakatwe.
Mkutano huo ukiendelea.


 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: