Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Watumishi Housing Investment (WHI) imeanzisha mfuko mpya wa uwekezaji wa pamoja unaoitwa FAIDA FUND ambayo unayalenga makundi yote ya kijamii,kwa lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji wa pamoja wakiwemo watoto, Wakulima, Wavuvi, Watumishi wa Umma, Wafanyakazi, Makampuni na Taasisi kuwekeza kwenye mfuko huo mpya.


MKURUGENZI Mtendaji wa taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI), Dkt.Fred Msemwa Amesema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, wakati akielezea utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko huo na kusema Faida Fund imeanzishwa chini ya sheria ya masoko ya mitaji na Dhamana sura ya 79 ya sheria ya Tanzania


Dkt.Msemwa amesema Faida Fund unafanya kazi kwa njia ya kuuza vipande, ambapo bei ya kipande ilikuwa sh 100, mpaka sasa thamani ya kipande imefikia sh 101.1, hivyo thamani ya vipande imeendelea kukua.


Amesema Wawekezaji wa Faida Fund wamefikia 4037 ambao wameonesha nia na 1348 wameshaanza kuwekeza hivyo mfuko huo umekubaliwa na watanzania wengi kwa muda mfupi tangu kuanziashwa kwake 1/11/2022 ambapo mfuko huo unatakribani miezi miwili. 



Akizungumzia uuzaji wa vipande mkurugenzi huyo amesema, Watumishi Houseng ndio wanaonunua vipande kutoka kwa wawekezaji ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaokuwa na uhitaji wa kuuza vipande vyao ili wapate Fedha.


Dk. Msemwa ametaja faida ya kuwekeza kwenye Mfuko, kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuwekeza katika masoko ya Fedha bila kulazimika kufuata mlolongo mrefu ikiwemo kwenda kwa madalali, uwekezaji hufanyika kwa njia ya simu hivyo kuokoa muda na kuwa na usalama wa fedha na kupata unafuu na kuwekeza bila tozo huku uwekezaji wako ukitambulika kwa Kasi kikubwa.


Pia amesema uwekezaji unaweza ukautumia kama dhamana pale utakapohitaji mkopo wa Benki ili kujiongeza zaidi kiuchumi na Mfuko wa faida fund ni endelevu na unalengwa sekta zote.


Amesema shirika kwa kushirikiana na Mamlaka za Elimu (TEA) imejenga nyumba186 Vijijini katika shule za kata zenye mazingira magumu na kuwa na manufaa makubwa katika kuwawezesha waalimu kuwa na makazi bora.


Kuhusu ujenzi wa nyumba amesema Nyumba 983  zimejengwa kupitia taasisi hiyo ya Watumishi Housing kwa mikoa 19 nchini na kwamba katika ujenzi wa kila nyumba 100 Watumishi Housing huzalisha ajira kwa watu 120.


WHI inamatarajio ya kuwa na miradi mipya ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Katika mikoa ya Day es salaam, Dodoma, Arusha USARIVER.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: