Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Baadhi ya Wakuu wa wilaya za mkoa wa Morogoro wakiwa katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa akizungumza katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mjini Rebecca Nsemwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo.

Mkurugenzi Msaidizi Urasimishaji Makazi holela Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nicholaus Mwakasege akiwasilisha mada ya mpango wa urasimishaji katika mkoa wa Morogoro wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI)

********************

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinatenga maeneo ya uwekezaji ili kurahisisha wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali bila usumbufu.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo tarehe 22 Februari 2023 wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika mkoani humo.

Waziri Mabula amesema, Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameifungua nchi kwa kukaribisha wawekezaji ambapo alieleza kuwa tayari wawekezaji wameanza kuja kwa wingi na kushindana kwenye sekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda , madini na ujenzi wa nyumba.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Rais Samia alielekeza kila halmashauri nchini kutenga maeneo ya uwekezaji hivyo ni jukumu la kila halmashauri kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanaandaliwa na kutengwa sambamba na kuwekewa mkakati utakaofanya maeneo hayo kuwa tayari kwa uwekezaji.

Akitolea mfano maeneo ya vijijini, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema kama vijijini maeneo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji basi mamlaka husika zihakikishe taratibu zote za kuhaulisha ardhi ikamilike na kusubiri wawekezaji na kuacha kusubiri muekezaji aje ndiyo waanze kuhangaika kuhangaika.

‘’Tunahitaji kuwa na ardhi tayari akitokea muwekezaji akija wa kilimo tunamuambia nenda kilosa, au nenda malinyi akifika anakuta ardhi iko tayari na asifike akaanza kugombana na wananchi.

Ametoa rai kwa halmashauri nchini kuwa ‘pro active’ kwa kutenga maeneo mapema na kwenda kuyamiliki na kubainisha kuwa kama ni halmashauri ya wilaya au kijiji au mwananchi mmoja mmoja mwenye ardhi yake ambaye halmashauri inamtambua basi eneo hilo liwe limetengwa mapema.

Amesema halmashauri zikifanya hivyo au kutekeleza hayo basi azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha nchi inasonga mbele katika masuala ya uwekezaji na kuondoa changamoto katika uwekezaji itakuwa imesaidia sana.

Aidha, Dkt Mabula alisema ni jukumu la viongozi wote kuanzia ngazi wilaya halmashauri hadi vijiji kuhakikisha wanasimamia na kutatua changamoto zote za migogoro ya ardhi katika maeneo yao na kubainisha kuwa mgogoro wa mpaka na mpaka siyo wa waziri kwenda kuutatua na unapaswa kutatuliwa katika ngazi husika.

Akigeukia suala la urasimishaji makazi holela Dkt Mabula alisema zoezi hilo siyo program ya kudumu na ilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na maeneo ambayo yalikuwa yameendelezwa bila kufuata taratibu za mipango miji. Programu ya urasimishaji makazi holela mwisho ni mwaka huu wa 2023.

Waziri Mabula amezielekeza mamlaka za upangaji nchini kuongeza nguvu ya kurasimisha mitaa yote iliyosalia na kuimarisha mikakati ya kuzuia ongezeko la makazi holela nchini ili kudhibiti ukuaji miji kiholela.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: