Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini Upendo Lugongo (katikati) akishuhudia utiaji wa saini mkataba wa maji  tayari kwaajili ya kwenda kutekeleza .,


Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba akikabidhi mkataba kwa mmoja wa wakandarasi wanaokwenda kuteleleza mikataba hiyo kwaajili ya kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Denis Chambi,  Tanga.

WAKALA wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) imesaini jumla ya mikataba 8 ya miradi ya maji itakayotekelezwa  katika wilaya  tano za mkoa huo  pamoja na mkataba mmoja wa mhandisi mshauri  itakayogharimu zaidi shilingi Bilion 10 ambayo inatarajiwa kuhudumia  wananchi katika vijiji 20 wapatao 39, 226 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2023 sawa na asilimia 1.5 ya wakazi wote wa mkoa huo.

Miradi hiyo ambayo ni mipya  yenye jumla ya vituo 92 vya kuchotea maji na matangi 9 yenye ujazo wa jumla ya mita za ujazo 1,  830 pamoja na mtandao wa mabomba kilometa 162.2 inatarajiwa kuongeza hali ya upatikanaji wa  huduma ya maji kwa asilimia 1.5 kwa wananchi wanaoishi vijijini.

Akizungumza meneja wa RUWASA mkoa wa Tanga Upendo Lugongo amesema kuwa lengo  la kusainiwa kwa mikataba hiyo ni  kuingia makubaliano ya pamoja na wakandarasi pamoja na mhandisi mshauri ambayo yataleta  ufanisi na tija ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kufuata kanuni , taratibu na sheria mbalimbali zitakazofuatwa kwa nia ya kukamilisha utekelezaji huo.

Alisema licha ya miradi hiyo mipya kusainiwa ipo mingine minne inatekelezwa  ikilenga kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji vijijini katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga ambapo jumla ya wananchi 2, 310000 wanatarajiwa kunufaika mara baada itakapokamilika.

"Kuna miradi mingine  mikubwa ambayo inaendelea miradi yote itakapokamilika itaenda kuwahudumia wananchi wapatao 2, 31000  sawasawa na asilimia 9 ya wakazi wa mkoa wa Tanga ukilinganisha na ile  ya mwaka 2022,   tunaenda kusaini mikataba 9 ambayo ni ndani ya ujenzi lakini pia kuna mkataba mmoja wa mhandisi mshauri  na katika mikataba hii nane tunaweka kwanza mabomba yenye jumla kilometa 1, 68, 000 ambayo  ina thamani yabshilingi  bilion 10 na inaenda kujenga vituo 110 ambavyo tutakuwa tunahudumia wakazi 31, 0000 "

"Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha   tunamtua mama ndoo kichwani na kuona kwamba huduma ya maji tunaenda kuitoa na kupunguza muda wa utafutaji maji  kwa wananchi ili  waweze kushiriki kwenye kazi nyingine za kiuchumi , serikali inaelekeza kuwa ifikapo 2025 tuwe tumefikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji vijijini" alisema Lugongo 

Akizungumza mara baada ya kusainiwa  kwa mikataba hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka wakandarasi wote watakaotekeleza miradi hiyo ambao wengi wao ni wazawa  kuwa wazalendo na kukamilisha kazi kwa wakati ili iweze kuleta tija  kwa wananchi akiwaelekeza pia kuwatumia wakazi wa maeneo husika kwenye kazi mbalimbali katika kipindi chote cha utekelezaji.

"Fedha hizi ni nyingi sana ambazo ni kodi za watanzania hivyo zinatakiwa zionyeshe matokeo makubwa yenye tija kwa miundombinu ya maji inayotumiwa na wananachi ili kukidhi malengo ya serikali, nimeelezwa kuwa  sehemu kubwa ya wakandarasi wanaotekeleza miradi hii ni wazawa hivyo nawataka kuwa wazalendo kwa kufanya kazi weledi na ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa mikataba hii nasisitiza wakandarasi kuwatumia wananchi wa maeneo  inayotekelezwa miradi hii katika kazi za vibarua ambazo hazihitaji utaalam mkubwa" alisema Mgumba.

Aidha Mgumba amewataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kuyatunza mazingira sambamba na kujiepusha na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ambapo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikichangia kukosekana kwa huduma hiyo na hatimaye kusababisha athari mbalimbali ikiwemo changamoto ya maji ya kutosha pamoja na ukame katika vyanzo vikubwa vinavyotegemewa na mamlaka husika.

"Kuna changamoto ya upatikanaji wa maji safi na yamekuwa haba ni kwa sababu ya ukame ambao umesababishwa na uharibifu wa mazingira na  ukame  ikiwemo shughuli za kibinadamu na kuvamia vyanzo vya maji nitoe wito kwa wananchi tutunze mazingira ili nayo yatutunze  ili kuondokana na uhaba huu wa maji ili mito yetu iwe na maji muda wote"

"Tuna tatizo kubwa la uhaba wa maji katika mkoa wetu wa Tanga  na moja wapo ya sababu ni kutokana na umeme mdogo tuliokuwa nao unakatika mara kwa mara na hautabiriki kwahiyo tuna uhaba zaid ya Mega wat 20 zinazohitajika  mahitaji yetu yalikuwa zaid ya megawa 136 lakini sasa zimeshuka hadi 80" alibainisha Mgumba 

RUWASA  mkoa wa Tanga imeingia makubaliano na makambuni mbalimbali ambayo ni kampuni ya Nipo Africa engineering Co.ltd atakayetekeleza miradi katika wilaya ya Kilindi ,  Lukedan Company Limited wilaya ya Handeni,  Wraptec engineering ltd Handeni, Planet water Geographycs ltd (Mkinga),  Wraptec engineering ltd (Korogwe),  Buzubona and Sons Company  na Hinry Company (Lushoto) pamoja na kampuni ya  Env Consultant.Share To:

Post A Comment: