Na Denis Chambi, Tanga.

 SAID Kibula   mwenye umri wa miaka 69 ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa 8 wa tukio la wizi wa mali mbalimbali katika ajali  iliyotokea hivi karibuni wilayani Korogwe mkoani  Tanga ikihusisha gari aina ya Fuso iliyogongana na Coaster iliyobeba mwili wa marehemu  pamoja na waombolezaji wakitokea mkoani Dar es salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwaajili ya mazishi  amekutwa amejinyonga  na Chandarua nyumbani kwake usiku wa february 22,2023 .

Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga ACP David Chidindi  amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Magira Gereza alikwa nje kwa dhamana  ya mahakama ya hakimu mkazi Korogwe.

Itakumbukwa kuwa  manamo February 3,2023  katika eneo la Magira Gereza tarafa ya Mombo wilayani Korogwe mkoani Tanga ilitokea ajali hiyo  iliyopelekea vifo vya watu 17 na  majeruhi 12  ambapo baadaye vifo viliongezeka na kufikia 21  wengi wao wakiwa ni wa familiya moja .

Wakati wa kuagwa kwa miili hiyo mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo aliibuka na kueleza namna alivyoshuhudia baadhi ya waokoaji walivyowaibia wahanga mali mbalimbali zikiwemo simu, nguo na fedha walizokuwa wamebeba .

 Kufwatia  ushuhuda huo  serikali ilitoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama  kuwasaka watumiwa hao ambapo walifanikiwa kuwakamata watu 12 na kati yao 8 walikutwa na hatia.

 Akieleza kuhusiana na tukio hilo mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema  kuwa mmoja kati ya watuhumiwa 8 aliyekutwa na nguo  za marehemu zikiwa na damu usiku wa kuamia alhamis  ya february 23 amekutwa  amejinyonga nyumbani kwake ,   ambapo sasa wamebaki saba ambao wapo kwenye mkono wa sheria.

"Tulipata msiba wa ajali ya gari  wiki kadhaa zilizopita lakini jambo la aibu lilitokea  kwa majeruhi  na marehemu kuibiwa vitu  vyao na watu wote 12  tumewakamata  na wanane  kati yao baada ya uchunguzi  ndio tuliwafikisha   katika vyombo vya sheria  na wapo mahakamani,  na kwa bahati mbaya sana mmoja wapo ambaye  tulimkamata akiwa na nguo za marehemu zikiwa na damu  na mali nyinginezo  ikiwemo simu za marehemu  (jumatano) amejinyonga  kwahiyo tumebaki na watu saba  lakini wapo kwenye vyombo vya sheria.

Share To:

Post A Comment: