Elizabeth Joseph,Monduli.


BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia  Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh, Suleiman Mwenda na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Mh,Joshua Nassari,leo Februari 23 2023 Mh,Mwenda amemkabidhi rasmi ofisi Mkuu mpya wa Wilaya hiyo Mh,Nassari.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo ambayo yalihudhuriwa na Wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama wilayani humo Mh,Mwenda licha ya kumpongeza Mh,Nassari kwa uteuzi pia alimuomba kuhakikisha anamaliza changamoto zote zinazoikabili Wilaya hiyo hasa changamoto ya migogoro ya mipaka ya Vijiji,Wilaya na Mkoa.

Mh,Mwenda pia aliwaomba Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Idara kuhakikisha wanampa ushirikiano katika kazi Mkuu mpya wa Wilaya hiyo ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa urahisi na hivyo kuleta maendeleo kwa wana Monduli.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh Joshua Nassari licha ya kushukuru kwa mapokezi alisisitiza suala la ushirikiano baina ya Watumishi wote hasa katika kutatua changamoto ya mipaka na malisho ya mifugo ili kwa pamoja waweze kupata utatuzi wa kudumu utakaoweza kulinda mifugo pamoja na kuongeza uchumi kwenye Wilaya hiyo.

Aidha Nassari aliwataka wakuu wa Idara hao kutekeleza majukumu yao iwapasavyo ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu katika ukusanyaji wa mapato ikiwa ni pamoja na kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuendelea kuongeza mapato katika Halmashauri hiyo.

"Tusiharibu mahusiano na ushirikiano wetu kwa kutotimiza wajibu ,kila mmoja atimize wajibu wake,nisingependa kufanya maamuzi yasiyotufurahisha hivyo tutembee pamoja kutatua changamoto za wananchi pamoja na kumsaidia Mheshiwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan"alisisitiza kusema Mh, Nassari.

Awali katika uteuzi uliofanyawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh,Dkt Samia Suluhu Hassan mwezi Januari mwaka huu alimteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba kuja Wilaya ya Monduli huku Mheshimiwa Joshua Nassari aliyekuwa Wilaya ya Bunda mkoani Mara akipelekwa Wilaya ya Iramba ambapo Mh,Mwenda anarudi kuendelea na majukumu yake Wilaya ya Iramba mkoani Singida.


Share To:

Post A Comment: