Na; Elizabeth Paulo, Dodoma

Baraza La Taifa Ujenzi limefanikiwa kuratibu,kuandaa na kuwasilisha Wizara ya ujenzi na uchukuzi(sekta ya ujenzi) andiko dhana (concept note) lenye mapendekezo ya kuboreshwa kwa mfumo wa sheria zinazosimamia ujenzi wa nyumba na majengo nchini.

Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa baraza la taifa la ujenzi Dk.Matiko Mturi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa baraza hilo katika serikali ya awamu ya sita.

Baraza la Taifa la ujenzi limeendesha mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi na utatuzi wa migogoro katika miradi ya ujenzi kwa wadau 155 kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani.

Aidha amesema wameandaa Rasimu ya Mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara (base unit rates) kwa kila mkoa wa Tanzania bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.

"Tunaendelea kuratibu utatuzi wa migogoro ya miradi ya ujenzi kwa njia ya adjudication na arbitration ambapo jumla ya mashauri 6 yametolewa uamuzi na 31 yanaendelea katika hatua mbalimbali za utatuzi" Amesema Dk.Mturi

Amesema Baraza limeendelea kuratibu utatuzi wa migogoro ya miradi ya ujenzi ambapo jumla ya mashauri sita yametolewa uamuzi huku mengine 31 yakiwa katika hatua mbalimbali za utatuzi.

Dkt.Mturi amesema kuwa wanatatua migogoro hiyo ikiwa ni sehemu ya majukumu yao kama baraza linaloshughulika na sekta ya ujenzi.

"Baraza la Taifa la ujenzi linatoa huduma mbalimbali kwa wadau wa sekta ya ujenzi ikiwemo uratibu wa sekta,ushauri wa masuala yoyote yanayohusu sekta ya ujenzi,uratibu wa usuluhishi wa migogoro katika sekta ya ujenzi,

"Kutoa mafunzo kwa wadau wa sekta ya ujenzi,ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya ujenzi,utafiti,ukusanyaji,uchapishaji na usambazaji wa taarifa za sekta ya ujenzi na miongozo mbalimbali ya gharama za ujenzi nchini,"amefafanua Dkt.Mturi.

Dkt.Mturi ameeleza kuwa kutokana na majukumu hayo wanayoshughulika nayo katika kipindi cha Julai 1,2022 hadi Januari 31, 2023 NCC imefanikiwa kutekeleza majukumu kadhaa ikiwemo kuandaa rasimu ya mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.

Pia ameeleza mipango ya utekelezaji kwa Februari 1, 2023 hadi Juni 30 ,2023 kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususan taasisi za umma zinazotekeleza miradi ya Miundombinu.

Pamoja na hayo Dkt.Mturi ameeleza kuwa lilihamasisha uundwaji wa bodi za usajili na vyama vya wadau wa sekta ya ujenzi likiwa na lengo la kutoa fursa kwa wataalam katika sekta ya ujenzi kutekeleza kazi zao kwa kuongozwa na mifumo iliyowekwa na Serikali pamoja na kulinda taaluma katika sekta hiyo.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: