Mkuu wa Wilaya ya Dodoma  Jabir Shekimweri akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mfuko Kuchochea Maendeleo wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo wameongoza zoezi la ugawaji wa vifaa vya kuchapishia mitihani ambavyo vitawekwa katika vituo vya umahiri vya majaribio ya mitihani katika tarafa zote 4 za Dodoma pamoja,fedha taslimu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pamoja na fedha za ujenzi wa kivuko cha wanafunzi.


Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Jiji Dodoma ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ambaye amempongeza Mbunge Mavunde kwa ubunifu mkubwa wa kuchochea maendeleo katika Jimbo la Dodoma Mjini na kuwataka watendaji wote kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa na fedha zinatumika vyema kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa.


Akitoa maelezo ya awali,Mbunge Mavunde alibainisha mambo yafuatayo;


-Shukrani kwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza fedha za mfuko wa Jimbo kutoka Tsh 70,000,000 mpaka Tsh 93,848,000 ambazo ndizo zimetumika kununua vifaa kwa wakati huu.


-Mfuko wa  Jimbo unajielekeza katika maeneo makubwa matatu ELIMU,AFYA & UWEZESHWAJI WANANCHI KIUCHUMI


-Kupitia Mfuko huu tunakwenda kuanzisha vituo mahiri vya majaribio kwa kila tarafa katika tarafa zote (4) nne kwa kuweka Computer Printer na Photocopier kwa kila kituo,hali ambayo itapunguza michango kwa wazazi kuchangia mitihani ya kila wiki.


-Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Kunambi,Mbuyuni-Kizota,Shule Mpya Ya Sekondari Matumbulu na Shule ya Msingi Michese-Mkonze.


-Ujenzi wa kivuko cha wanafunzi wa Sekondari ya Sechelela inayohudumu kata za Dodoma Makulu na Tambuka Reli.


Wakizungumza  katika hafla hiyo Meya wa Jiji la Dodoma *Prof Davis Mwamfupe * na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma *Ndg Joseph Mafuru* wameahidi kuunga mkono jitihada za Mbunge Mavunde kupitia mfuko wa Jimbo ili kupeleka maendeleo kwa haraka kwa wananchi wa Dodoma.


Wakati huo huo,Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini kupitia kwa Katibu Mwenezi wa Wilaya *Ndg. Amani Mulagizi* kimepongeza hatua hii ya utoaji wa taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kutoa maelekezo kwa viongozi wote wachaguliwa kueleza kwa uwazi mambo yote ya utekelezaji wa Ilani.

Share To:

Post A Comment: