Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Daud Yassin katikati akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa juu ya utekelezaji wa miradi ya Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Daud Yassin katikati akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego Iringa juu ya utekelezaji wa miradi ya iliyoainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi


Na Fredy Mgunda, Iringa.

CHAMA cha mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimewataka watendaji kutekeleza miradi yote kwa uadilifu mkubwa ili wananchi waendelee kukiamini chama hicho kila Kona.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Iringa mwenyekiti wa chama hicho, Daud Yassin Alisema kuwa
Kilichobaki ni kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kumuunga mkono Rais Samia 

Yassin amesema Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa imekagua Utekekezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuridhishwa na miradi waliyopitia.

Aidha Yassin amewataka watendaji kufanya kazi kwa uadilifu katika kuwatumikia wananchi badala ya kuwasubirisha kwa yake yanayowezekana kufanyika.

Akizungumza wakati akihitimisha ziara  hiyo baada ya kukagua miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Yasin alisema ili kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lazima watendaji wafanye kazi kwa bidii na weledi.

"Linalowezekana leo lisingoje kesho, kama Mwananchi amekuja kupata huduma na unaweza kumsaidia leo usimwambie aje kesho, mara njoo jumatatu, haipendezi," amesema Yasin na kuongeza;

"Kamati ya Siasa wamekagua miradi na wamesema wameridhishwa vinginevyo wangesema."

Alisema Rais Dkt Samia  ametoa fedha nyingi kwa ajili ya utekekezaji wa miradi mbalimba. hivyo ujenzi wa miradi hiyo lazima uendane na fedha zilizotolewa.

"Rais wetu anafanya kazi kubwa sana lazima tumuunge mkono," alisema.

Kamati hiyo ilipitia miradi mbalimbali katika Wilaya za Mufindi, Kilolo na Iringa.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: