Na mwandishi wetu,Malinyi

Madarasa 10 yaliyojengwa kwa fedha za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk.Samia Suluhu Hassan  maarufu kama fedha za mfuko wa kapu la mama yamefanikisha kuanza masomo wanafunzi wote  waliochaguliwa kujiunga kidato Cha kwanza wilayani Malinyi 2023.


Fedha hizo zilizotolewa Oktoba mosi mwaka 2022 zilikuwa na lengo la kupunguza uhaba wa madarasa katika Halmashauri zote sekondari za serikali  nchini ambapo halmashauri ya Malinyi ilipokea kiasi Cha shilingi milioni 200.


Mkuu wa Divisheni ya Elimu sekondari Halmashauri ya wilaya ya Malinyi Pendo Masalu amesema fedha hizo zimefanikisha ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa ambavyo vimeongeza idadi ya mahitaji halisi ya madarasa 11 yaliyokuwa yanahitajika.


Amesema madarasa yaliyojengwa katika fedha hizo yamekamilika kwa asilimia 100 na samani zake na wanafunzi wameshaanza kuyatumia  katika masomo.


Amezitaja shule zilizofaidika na fedha za kapu la mama ni Sekondari  za Itete, Njiwa,Usangule, Mtimbira,Sofi,Kipingo,Malinyi,Igawa,Biro na Kilosa Mpepo.


"Kwanza ninashukuru Mheshimiwa Rais kwa fedha hizo zimetusaidia sana katika kupunguza uhaba wa madarasa na sisi Malinyi tumezitendea haki kwa kujenga madarasa bora ambayo watoto wetu wameanza kuyatumia katika muhula huu wa masomo wa 2023".


"Kwa pekee nawapongeze pia walimu wetu kwa usimamizi mzuri wa ujenzi  na matumizi mazuri ya fedha wakishirikiana na  kamati zao za ujenzi katika utekelazajj wake kila mtu alikuwa mwadilifu "alisema Pendo Masalu.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa divisheni ya Elimu sekondari madarasa hayo yatapokea wanafunzi 2746 ambao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shule za sekondari za kutwa Malinyi mwaka 2023.


Kati ya wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza mwaka huu walioripoti mpaka kufikia February 22 ni 2625 sawa na asilimia 96.


"Nawashukuru sana a watendaji wa serikali walioshiriki katika ujenzi huu kamati ya ulinzi na usalama, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Malinyi ,mhandisi wa ujenzi,afisa manunuzi,muhasibu wa wilaya wote walishiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa ujenzi"alisema Pendo.





MWISHO.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: