Na Farida Mangube Morogoro 



WANAWAKE nchini wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika harakati za utunzaji wa vyanzo vya maji lengo likiwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.


Ushauri huo umetolewa na wadau mbalimbali waliokutana mkoani Morogoro kwenye semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Shahidii wa Maji kupitia programu yake ya Paza Sauti.


Miongoni mwa wadau walioshiriki semina hiyo ni waandishi wa habari, tasisi za kiraia pamoja na Mashahidi wa Maji ambapo wanaharakati wa kutetea na kupinga uharibifu wa rasilimali za maji huku wakitukumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa wanawake kuwa mstari wa mbele katima utunzaji wa mazingira na kupaza sauti kwenye changamoto ya upatikanaji wa maji.


Akizungumza katika mkutano huo Mmoja wa wanaharakati hao Gemma Akilimali amesema wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa Maji hivyo endapo watashirikishwa ipasavyo itasaidia kwani ndio watumiji wakubwa wanatambua umuhimu wake.


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shahidi wa Maji Abel Dugange amesema bado jamii inafumbia macho tabia ya uharibifu wa mazingira na rasilimali maji kwenye maeneo yao hali inayosababisha baadhi ya maeneo kukosa maji safi na salama.


" Kwenye ngazi ya jamii tunatarajia kwamba ingekuwa mstari wa mbele katika kuibua changamoto na kuhakikisha inasimamia kikamilifu kupitia kamati za mazingira na mwananchi mmoja mmoja lakini tunaona bado kuna hali fulani ya kufumbiana macho na wengine bado wanalima mpaka kwenye kingo ya mto na hakuna anayetoa taarifa na viongozi wapo,"ameema.


Aidha amewataka Watanzania kutambua kuwa usalama wa nchi unachagizwa na usalama wa maji hivyo kila mmoja anawajibu wa kulinda na kutinza vyanzo vya maji kwani mwananchi akikosa maji safi na salama maisha yake yanakuwa hatarini.


Pia amesema mpaka sasa Shirika hilo limeendelea kuwajengea uelewa zaidi wananchi kuhusu kutambua wajibu wao katika kutunza mazingira na vyanzo vya maji lakini wamekuwa wakielemisha kuhusu mambo ya kisheria kwenye eneo la rasilimali maji katika mikoa mbalimbali.



Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: