Baadhi ya viongozi wa timu zitakazoshiriki  michuano ya ligi ya Mafitha Cup wakiwa kwenye kikao cha pamoja na muandaaji wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kurindima jumatano hii jijini Tanga.

Na Denis Chambi, Tanga.

Jumla ya yimu 20 za mpira wa miguu  kutoka viunga mbalimbali vya jiji la tanga zitachuana kumtafuta bingwa wa ligi ya Mafitath Super Cup msimu wa 2023 ambaye anatarajiwa kuondoka na  Mbuzi,  jezi seti moja pamoja na mipira miwili.

Utepe wa michuano hiyo utakatwa jumatano hii  katika  uwanja wa Kombezi zikikutana timu mbili za kundi A ambazo ni  Pongwe Young Stars dhidi ya Mwambani FC wakianza kuzichanga karata zao kusaka kwa udi na uvumba ubingwa wa ligi hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa katika viwanja viwili ikianzia hatua ya makundi..

Akizungumza muandaaji wa ligi hiyo na mdau wa michezo jijini Tanga Mzamiru Yusuph alisema licha ya kuinua vipaji vya mchezo huo kwa vijana wanaoonekana kuvutiwa na kandanda kwa  sasa lakini pia wamedhamiria kupenyeza ujumbe kwao vwa kwa kutoa elimu na kuhamasisha kuondokana na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kujiepusha na makundi hatatishi hali ambayo kwa sasa inaonekana wimbi kubwa la  vijana kujiingiza katika vitendo hatarishi vinavyochangia pia mmomonyoko wa maadili.

"Ligi yetu imelenga kwanza kuhamasiaha mchezo wa  mpira  wa miguu kukuza vipaji kwa vijana wetu kujenga urafiki baina ya timu zilizopo lakini pia hizi timu iwe ni sehemu yao kupata wachezaji wazuri ili kuimarisha timu zao,  Lakini wakati huo tukasema hawa vijana wanapaswa wakumbushwe mambo ya msingi katika taifa letu ikiwemo kujenga uchumi binafsi, kama  tunavyofahamu  mpira  una uwezo wa kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja "

"Lakini pia kupitia ligi yetu iwakumbushe kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya athari zake tunazifahamu na wakati mwingine wahanga wakubwa ni vijana wetu tukaona tufikishe ujumbe  ambao utasaidia kujenga jamii yetu yenye amani na maadili mema" alisema  Yusuph.

Alisema nyuma ya waandaaji wa Mafitha Cup wapo wadau na  wapenzi soka ambao kwa pamoja kuna jambo  wameliandaa litakalokuja kuneemesha kila timu ambayo itashiriki michuano hiyo ambalo litakwenda kuzidi kuamsha ari kwa vijana wapenda soka jijini Tanga

"Kuna jambo ambalo tumeamua kulifanya  kwa timu zote ambazo zitashiriki tumepanga  tuje tuzione na zawadi ambazo zinatoka kwa wale ambao wameandaa Mafitha Cup hii ni tofauti na zawadi ambayo itatolewa baada ya ligi,  na  hii imelenga kutambua mchango wao katika mpira wa miguu"

"Mshidi wa kwanza tutampatia  Mbuzi , jezi pamoja na mipira miwili, mshindi wa pili tutampatia jezi na mpira mmoja wa tatu atapata jezi peke yake ,  mshindi wa nafasi ya nne na tano watapata mpira moja mmoja lakini hizi timu nyingine shiriki tunatarajia na wao pia hatutawaacha hivihivi tutawapatia baadhi ya vifaa vya mazoezi"

Mafitha Super Cup mwaka huu wa 2023 itazihusiaha timu za kundi A ambazo ni Pongwe Young Stars,  Mwambani FC,  Young Boys, Home Guard,  na Kiomoni FC huku kundi B likizibameba Kigongo FC,  Mitumba FC, Kange Stars,  Tanga Kwanza pamoja na Pongwe Stars.

Huku kundi C likiwa limesheheni vijana wa timu za Sigasiga FC,  Makorora Stars,  United Warriours,  Tanga United pamoja na TFC na D likizihusisha The City,  Tallent FC,  Magomeni FC,  Dandii na Middle FC ligi hiyo ikitarajiwa kutamatika mwezi March 2023 kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Share To:

Post A Comment: