Mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy akiongea Mara baada ya mkuu wa wilaya ya Mufindi kuapishwa mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Veronica kessy amewaomba wananchi na viongozi mbalimbali wa Iringa kumpa ushirikiano katika kazi ili kuleta maendeleo ya kukuza uchumi katika wilaya hiyo.
Kessy alisema kuwa wilaya ya Iringa inawananchi wachapakazi na wapenda maendeleo kwa kujituma kufanya kazi kwa kutumia mbinu mbalimbali za kiuchumi.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa ni mkoa mkubwa na wenye wananchi wapenda maendeleo hivyo anakuja kutoa ushirikiano kuhakikisha wanaendeleza kukuza uchumi wa wananchi wa Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Aidha mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy aliwaomba watumishi wa wilaya ya Iringa kutoa ushirikiano kuhakikisha wanasukuma maendeleo ya wananchi na kukuza uchumi wa wananchi
Kessy alimalizia kwa kumushukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kumuamini katika nafasi ya kuwa wilaya ya Iringa na amekuja Iringa kuwatumikia wananchi wa Iringa.
Post A Comment: