Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Kutokana na kukithiri Kwa uchafuzi wa Mazingira unaotokana na kelele na mitetemo Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mheshimiwa Seleman Jafo ametoa siku saba  (7) kwa wamiliki wa maeneo yote yanayofanya uchafuzi huo kurekebisha utoaji wa huduma zao ili ziendane na takwa la sheria ya mazingira na kanuni zake.


Jafo ametoa agizo hilo Leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  na kuagiza baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kufungia maeneo yote yatakayokaidi kutekeleza sheria na kanuni za Mazingira kuhusu kelele na mitetemo.


Kwa mujibu wa Mheshimiwa Jafo sheria ya Mazingira ya 191 Kifungu cha 106 Kifungu kidogo cha (5 na 6) kinakataza kupiga kelele kuzidi viwango vinavyoruhusiwa na vilevile ni kosa kupiga kelele kinyume na viwango vilivyoruhusiwa.


Aidha kanuni za udhibiti wa kelele na mitetemo za mwaka 2015 zimeainisha viwango vya sauti vinavyoruhusiwakwenye maeneo ya makazi,Biashara, Viwanda na Hospitali ili kulinda afya ya jamii. 

 

Jaffo amesema hatua za kisheria zilizoainishwa kwenye sheria ni pamoja na kutozwa faini na kufungiwa biashara kwenye maeneo yaliyokithiri kwa kelele na mitetemo.


Amesema pamoja na kuchukua hatua hizo za kisheria kumekua na ongezeko la malalamiko ya kelele na mitetemo kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 ambapo asilimia 65 ya malalamiko yaliyowasilishwa na baraza la mazingira yanahusu kelele na mitetemo hali inayoonyesha adhabu za kutozwa faini hazitoshi kwa wanaokamatwa.


Jaffo ametaja baadhi ya  maeneo yaliyobainishwa na  chombo cha usimamizi wa sheria ya Mazingira NEMC yenye kuendelea na uchafuzi wa Mazingira uliokithiri kuwa ni pamoja na Kipong bar and lounge kilichopo mkoani Arusha,Smart pack lounge (bar and lounge) Kilichopo Dar es salaam, Lapatrona bar kilichopo Dodoma na maeneo mengine mengi yanayoendeleza makelele na mitetemo.

Share To:

Post A Comment: