WATOTO wanaoishi kwenye kituo cha  Kindness Children Care kilichopo eneo la Kijenge, Arusha wamepewa elimu ya ujasiriamali wa kutengeneza batiki, sabuni , mafuta ya kujipaka  sanjari na misaada mbalimbali ya kijamii.

Mafunzo hayo yametolewa leo jijini Arusha katika makao ya watoto hao wapatao 45, ambao wengine wanasoma vyuo vya kati na wengine wanasoma shule za sekondari na msingi pamoja na watoto wawili wenye ulemavu.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili watoto hao, mlezi wa kituo hicho, Christina Yohana, amesema kituo kinakabiliwa na changamoto ya ulipaji wa kodi, kwani nyumbani waliyopo wamepanga, pia ada za watoto hao na huduma nyingine muhimu za kibinadamu.

“Naomba jamii itusaidie kwani hapa tulipo tunadaiwa kodi hatujui tutapata wapi fedha na ada za watoto hawa, tunaomba anayeguswa atusaidie hatuna wafadhili. Tunawashuku marafiki wa Cholobi kupitia taasisi ya Cholobi Foundation kwa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watoto hawa, kula chakula cha pamoja na kutoa misaada kwa watoto hawa mungu awabariki sana,” amesema.

Naye Ofisa Tarafa wa Elerai kupitia Taasisi ya Cholobi Foundation,Titho Cholobi amesema taasisi hiyo kupitia kwa marafiki zake wameungana pamoja kuuaga mwaka kwa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watoto hao, kula chakula cha pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii, ili kuwasaidia wanapomaliza masomo yao waweze kujikwamua kiuchumi.

Share To:

Post A Comment: