Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wanaoharibu chanzo cha maji  Endallah katika Kata ya Endamarariek Wilayani Karatu kwa kukata miti na kulima katika chanzo hicho.

Zelothe ametoa agizo wakati wa sherehe za miaka 46 ya CCM ambapo walifanya shughuli katika chanzo hicho ya kupanda miti eneo linalozunguka chanzo hicho.

"Tunapokata miti ya asili tunafanya maisha yetu kuwa magumu na vyanzo vya maji vinategemea uhifadhi wa misitu ya asili, inashangaza watu wanafyeka miti hadi kwenye vyanzo vya maji  kwa ajili ya shughuli za kilimo" Zelothe 

 Pia Zelothe amewaomba wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya CCM kutokana na jitihada kubwa inazozifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali.

“Tunapotimiza miaka 46 ya CCM naomba wananchi wa Karatu hususani Kata hii ya Endamarariek muendelee kuiamini serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikileta fedha nyingi katika wilaya hii ya Karatu kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, miundombinu".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Simon Maximillan Iraghe amesema CCM imefanya mambo mengi yanayoonekana kwa macho huku serikali ikiwekeza fedha nyingi na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa kipo kazini kuhakikisha kinatatua matatizo ya wananchi


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akishiriki ujenzi wa jengo la Umoja wa Wanawake UWT  tawi la Khusumay ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Arusha Simon Maximillan Iraghe sambamba na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa Tezra Semuguruka Wakishiriki ujenzi wa jengo la Umoja wa Wanawake UWT  tawi la Khusumay ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Mkoa wa Arusha Bi, Flora Zelothe akipanda mti katika Shule ya Sekondari Khusumay ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM (MNEC) kutokea Mkoa wa Arusha Dkt, Daniel Pallangyo akipanda mti katika Shule ya Sekondari Khusumay ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Arusha Simon Maximillan Iraghe akipanda mti katika Chanzo cha maji cha Endallah ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Share To:

Post A Comment: