Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas akiongea na wananchi wa Mkoa wa Iringa wakati wa uzinduzi wa miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi na kutoa ahadi ya ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Kiyowela.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas.Na Fredy Mgunda, Iringa.


CHAMA cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kimepanga kutatua changamoto uhaba wa bweni katika shule ya sekondari ya kiyowela ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa kwa Watoto wa kike.


Akizungumza wakati uzinduzi wa maazimisho ya miaka 46 ya chama hicho,Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas alisema kuwa amesikia kero iliyosemwa na Diwani wa kata ya kiyowela ya uhaba wa bweni la shule ya sekondari Kiyowela.

Asas alisema kuwa yupo tayari kuchangia ujenzi wa bweni hilo hata kwa asilimia 90 ilimradi kuwawezesha wanafunzi hasa wa kike kusoma wakiwa bwenini.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa kimepanga kuboresha sekta ya elimu hivyo uongozi wa kata na shule hiyo wanatakuwa kutuma haraka michoro ya ujenzi wa bweni hilo ili waanze ujenzi mara moja.

Asas alimpongeza MNEC Qwihaya kwa kujitolea Tripu 20 za tofari kwa ajili ya ujenzi wa bweli la shule ya sekondari Kiyowela jambo ambalo linatakiwa kuigwa na wanaccm na wananchi wote.

Alisema kuwa anachangia ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Kiyowela ili kuwanusuru wanafunzi wa kike wanaotembea zaidi ya kilometa saba kwenda shuleni.

Awali Diwani wa Kata ya Kiyowela, Steven Muhumba alisema katika mkutano huo kwamba ukosefu wa bweni katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 400 unawaweka wanafunzi hasa wasichana katika mazingira hatarishi na akaomba msaada wa ujenzi wa bweni litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200.

Kwa upande wake Qwihaya aliahidi kuchangia tripu 20 za tofari kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo huku Mkuu wa Mkoa akisema serikali itaweka pia mkono wake katika shughuli hiyo.

“Qwihaya ameahidi tripu 20 na serikali ya mkoa imesema itaweka mkono wake; mimi naahidi sehemu yote itakayobaki katika ujenzi wa bweni hilo, nitaikamilisha,” Asas alisema na kuamsha vigelegele kutoka kwa wananchi.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: