Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) leo Januari mosi 2023, imeanza rasmi shughuli zote za uendeshaji wa kitengo cha makasha cha gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salam.

Hatua hiyo ni kufuatia kukoma kwa ndoa baina ya mamlaka hiyo Jana Jumamosi, Desemba 31, 2022 na Kampuni binafsi ya kimataifa ya kuhudumia makontena Tanzania (TICTS) iliyodumu kwa takribani miaka 22.

Licha ya kuwepo kwa kipengele kinachowaruhusu wawili hao kuendeleza mahusiano hayo kama ilivyokuwa Julai 6, 2017 ambapo walikubaliana kuendela kufanya kazi kwa miaka mitano hadi Septemba 30, 2022, TPA haikuridhia kwa mara nyingine na  kuendelea na huduma za kampuni hiyo Desemba 31, TICTS kukabidhi majukumu kwa TPA.

Leo Januari mosi , 2023  TPA kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wake, Plasduce Mbossa imesema kutokana na mabadiliko hayo kila mteja mwenye mzigo  uliokuwa chini ya eneo lililokuwa likihudumiwa na TICTS na watakaoleta mizigo kupitia gari namba 8 na 11 za Bandari ya Dar es Salaam atapaswa kufanya malipo yote ya gharama  za huduma za Bandari.

Malipo hayo yatafanyika kwa kutumia mwongozo wa gharama za bandari  uliokuwa ukitumiw ana TICTS kupitia benki TPA 7045004906 Swift Code ECOCTZCTZ au Stnadrd Charted 01-080-921638-01Swift Code SCBLTZTXXXX.

”Katika kipindi hiki cha mpito, anuani za mawasiliano na ofisi ambazo zitatumika kutoa huduma zitaendelea kuwa kama ambavyo ilikuwa ikifanyika wakati wa uendeshaji wa shughuli za kampuni ya TICTS hadi pale utaratibu mpya utakapotolewa,” imeeleza taarifa hiyo.

Share To:

Post A Comment: