Na John Walter-Babati


Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, imemhukumu  Richard Martin  (42), mkazi wa kiijiji Cha Minjingu kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka binti wa miaka (11).

 

Hukumu hiyo imetolewa leo Januari 05/2023 mbele ya Hakimu Victor Kimario wa Mahakama ya wilaya ya Babati ambapo mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo 02/072022 huko katika kijiji cha Minjingu jirani na Ziwa Manyara.

 

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Mshtakiwa alimkuta mtoto huyo akiwa na kaka yake(14)  wakichunga ng'ombe ndipo akaomba kusaidiwa kwenda kupakiza gunia la mkaa, mtoto huyo na kaka yake walikubali kwenda kumsaidia lakini baada ya kufika njiani mshtakiwa alimwambia kaka wa binti kwamba  arudi kuangalia mifugo isipotee ndipo akaondoka na binti huyo kwenda kumbaka.

 

Majibu ya Uchunguzi wa daktari baada ya kumpima mtoto huyo yalithibitisha kufanyiwa kitendo hicho huku akiwa na maumivu makali ambapo walimpatia dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

 

Mwendesha mashtaka wa Serikali Grace Mgaya ameiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa mshtakiwa pamoja na wengine wenye tabia kama hiyo huku Mshtakiwa akiiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ana watoto watatu ambao ni wadogo na mama yao alishafariki hivyo wanamtegemea. 

 

Imeelezwa kwamba Mshtakiwa huyo aliieleza Mahakama kuwa 'Nilikuwa natembea nikakutana na Binti wa Miaka kati ya 10 na 11 akiwa na wenzake wanachunga ng'ombe,  nikaongea nae nikamwambia nataka penzi lako ambapo alikubali nikamuuingizia na kummwagia shahawa mara Moja

 

Mshtakiwa aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana watoto watatu wadogo na mama yao amefariki na kwamba wazazi wake ni wazee wanamtegemea.

 

Hata hivyo hakimu Kimario amesema mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Share To:

Post A Comment: