Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Dismas Prosper kushoto akimkabidhi pikipiki  mshindi wa droo  iliyopita ya mastabata kotokote Ally Abdallah katika tawi la benki hiyo Madaraka jijini .


Na Denis Chambi, Tanga.

BENKI ya NMB kupitia kampeni yake ya Mastabat kotekote imeendelea kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja wake wanaotumia huduma za kifedha kupitia Kadi(Master Kadi) ambapo shilingi Milion 59 hutolewa kila mwezi kwa washindi huku mshindi mmoja akijinyakulia pikipiki aina ya Boxer yenye thamani ya shilingi Million tatu mara baada ya droo kuchezeshwa. 

Akizungumza meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Dismas Prosper kwenye droo ya pili iliyochezeshwa leo katika tawi la Madaraka jijini Tanga amesema kuwa ni kawaida yao kurudisha faida kwa jamii ambapo wametenga zaidi ya shilingi Million 300 zitakazotolewa kwa wateja 854 katika kampeni hiyo ambayo itaendeshwa ndani ya wiki 10 kila wiki wakitoka washindi 75 na kujinyakulia shilingi laki moja moja na wengine 49 wakijinyakulia milion moja moja kila mwezi.

 "Huu ni mwaka wa nne wa kampeni za kuhamasisha matumizi ya kadi na mastabata QR, ili kurudisha faida tunayoipata kama benki kwa wateja wetu promosheni hii itashuhudia zawadi ya pesa tathlimu pikipiki pamoja na safari ya kuelekea Dubai kwa siku nne huku zawadi za pesa tathlimu zikiwekwa kwenye akaunti za wateja wetu ili kuhamasisha waendelee kufanya malipo kwa kadi zao" alisema Prosper

 "Kwenye kampeni hii shilingi Million 300 zitatolewa kama zawadi kwa washindi 804 kampeni hii inaendeshwa ndani ya wiki kumi kila wiki washidi 75 watapokea zawadi shilingi laki moja kila mmoja na mshidi mmoja atajishindia pikipiki huku 49 wakijinyakulia shilingi millioni moja moja kila mwisho wa mwezi kwa miezi miwili na mshindi mmoja kujinyakulia pikipiki katika kuhitimisha kampeni hii washindi saba watajinyakulia tiketi za kusafiri kuelekea Dubai pamoja na wenzi wao kwa siku 4 safari ambayo itagharamiwa kila kitu na benki ya NMB" alisema Meneja huyo. 

"NMB tunaendelea kuhamaisha wateja wetu kuwa kadi zetu sio tu kwaajili ya kutolea pesa katika mashine za ATM bali katika matumizi mbalimbali kama kufanya malipo ya Scan QR kwa kulipa mkononi katika sehemu za migahawa , Supermarket vituo vya mafuta na hata kuagiza bidhaa mbalimbali kupitia mitandao" aliongeza. 

Promosheni hiyo ya Mastabata Kotekote ilizinduliwa rasmi october , 2022 ikiwa mwaka huu 2023 ni wa nne katika kuhamasisha wateja wake kutumia miamala ya fedha kupitia kadi zao za Kibenki ili kurudisha faida wanayoipata kama benki.

 Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya bahati Elibariki Sengasenga katika halfa kugawa zawadi kwa washindi alisema kuwa bodi hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na kampuni zote zinazoendesha michezo yote ya kubahatisha hapa nchini ambapo inahakikisha kuwa sheria kanuni na masharti yote yanayoongoza michezo hiyo yanazingatiwa.

 "Kazi yetu sisi ni kutoa leseni kwa michezo hii ya kubahatisha lakini pia kuratibu mchakato mzima wa kutafuta washindi, kampeni hii inayoendeshwa na benki ya NMB ina viashiria vya bahati nasibu kwasababu washindi wanatafutwa kwa usawa hii inaonyesha jinsi gani NMB wanaifanya kampeni hii kwa usawa kabisa " alisema Sengasenga. 

Benki hiyo ya NMB leo katika tawi la Madaraka lililopo jijini Tanga imemkabidhi mshindi wa droo ya mwezi uliyopita Ally Abdallah mkazi wa mkoani hapa aliyejinyakulia pikipiki aina ya Boxer yenye thamani ya Shilingi Million tatu huku mshindi wa droo ya mwezi huu akiwa ni Emmanuel Malimbo kutoka Tabora. 

Mara baada ya kupokea zawadi yake mshindi wa droo iliyopita Ally Abdallah alisema kuwa amekuwa akitumia huduma za malipo kupitia Masterkadi za NMB katika biashara zake huku akijipanga zaidi kuendelea kufanya miamala ili aweze kujishindia tiketi ya kwenda Dubai kwa droo zinazokuja. 

"Nilipigiwa na wahudumu wa NMB kwamba nmeshinda kwakweli nilikuwa kidogo siamini amini kwa sababu ya mambo ya kiutapeli ambayo yameingia lakini nashukuru baadaye niliamini, mimi natumia sana master kadi kwaajili ya kulipa malipo mbalimbali katika biashara zetu, bado naendelea kupambana ili nipate ile ya Dubai." alisema Abdallah.
Share To:

Post A Comment: