Mkuu wa wilaya  ya Ikungi Mkoani Singida Jerry C. Muro amefanya ziara ya mwisho ya ukaguzi wa miradi miwili ya  maji katika kata za mtunduru na Irisya ndani ya Jimbo la Singida Magharibi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uzinduzi wa miradi hiyo ambapo uzinduzi utafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Dc Muro amejiridhisha kuwa miradi imekamilika na wananchi wameanza kuyatumia maji safi na salama na kuwaomba wananchi wa kila eneo lenye mradi kujitokeza kwa wingi kesho

Awali meneja wa Ruwasa wilaya ya Ikungi Mhandisi Hope Liundi amefafanua kuwa kila mradi umetengenezwa kulingana na mahitaji ya eneo husika ambapo amesema katika kata ya mtunduru mradi utanufaisha wananchi zaidi ya elfu tano mia nane na mradi utakuwa na uwezo wa kutoa zaidi ya lita laki moja na elfu kumi na saba kwa siku uku ukiwa na maeneo ya wazi ya kuchotea maji saba DP's kwa kuanzia

Mhandisi Hope pia amesema mradi wa maji wa irisya utanufaisha wananchi zaidi ya elfu tatu na mia nane uku ukiwa na uwezo wa kuzalisha lita zaidi ya laki mbili na elfu arobaini kwa siku ambapo chanzo chake ni kisima kirefu na umechukua muda wa miezi sita kukamilika 

Mhe. Muro amehitimisha ziara yake kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya hiyo kupewa fedha zaidi ya bilioni 2 kwenye sekta ya maji ikungi na kuwahakikisha viongozi wa halmashauri za vijiji vyote viwili ambavyo ni wanufaika kuwa watafanya kila linalowezekana kuhakikisha mpaka mwaka 2025 wanafikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji kutoka asilimia 62 za sasa hivi 


Share To:

Post A Comment: