MBUNGE wa Jimbo la Msalala Mhe.Iddi Kassim Iddi amekabidhi Jengo la chama la CCM Msalala Kwa uongozi wa CCM wilaya ambapo Kwa niaba ya Uongozi Katibu Wa CCM wilaya ya Kahama Cde. Mary Mhoha na Katibu Mwenezi Cde.Johachim Simbila walishiriki makabidhiano hayo.Mhe.Iddi Kassim Iddi ameahidi kumalizia ujenzi huo Kwa 100%, ikumbukwe kuwa Mhe.Iddi Kassim Iddi alijitolea kujenga jengo Hilo Kwa jitihada binafsi.


Aidha, Katibu Wa CCM wilaya ya kahama amempongeza Mhe.Iddi Kassim Iddi Kwani amekamilisha asilimia 90% za ujenzi. Pia, amewaomba wanachama wa Kata za Segese na Mega kushirikiana  kufanya usafi katika jengo la chama Kwa kuwa kilele Cha maadhimisho ya Sherehe ya miaka 46 ya Kuzaliwa Kwa CCM kimkoa yatafanyikia katika Jengo la CCM  Msalala.


Tukio Hili pia limehudhuriwa na Diwani wa Kata ya Segese Mhe.Joseph Manyara, Mwenyekiti mstaafu Uvccm shinyanga Cde.Baraka Shemahonge na Viongozi wa chama Kata na matawi Jimbo la Msalala.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: