Na Denis Chambi, Tanga.

Nyota wa zamani wa ngumi za kulipwa hapa nchini Rashid Matumla 'Snake man' amempongeza bondia Karim Mandonga kutokana na aina yake ya tofauti ya kuhamasisha inayomfanya kuwa kivutio kwa mashabiki na wapenzi wa ngumi Tanzania huku akimtaka kujipanga zaidi kwani anaweza kufika mbali zaidi kama tu ataendelea kucheza mapambano na mabondia wengi tofauti tofauti. 

Matumla ambaye ni bingwa wa dunia alimpongeza Karim Mandonga kufwatia ushindi wa KO alioupata nchini Kenya mbele ya mpinzani wake Daniel Wanyonyi katika Pambano lao akisema kuwa ni bondia wa kipekee ambaye atakuja kuvuma ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kama atajikita zaidi kibiashara kupitia mchezo huo. 

"Tathnia ya ngumi sasa hivi ni nzuri na inakuwa kusema kweli tunaona sasa ivi imezalisha mabondia wengi  na wa zuri , na sasa ngumi ziko juu ukitofautisha na kipindi hicho, kwa mfano sasa hivi tunamuona bondia Mandonga watu wengi anawafurahisha tunaona vile anavyotambulisha ngumi zake kwa majina tofauti tofauti amekuja na staili yake ya kipekee , kwahiyo Mandonga sio mtu wa kumdharau hata Kidogo.

" Akizungumza mkoani Tanga kuelekea mapambano ya january 18 na 28 mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Promota Ally Mwazoa ambapo watashuhudiwa mabondia mbalimbali wakipanda ulingoni kuzichapa, Matumla amesema kuwa wapo vijana wengi sasa hivi wameonekana kuvutiwa na kuhamasika kujiingiza katika mchezo wa ngumi za kulipwa hatua ambayo inapaswa kuungwa mkono na kupewa kipaumbele hasa  wadhamini mbalimbali kujitokeza kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na vipaji vingi vya ngumi.
Share To:

Post A Comment: