Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, wakati alipofanya ukaguzi wa hali ya hifadhi ya usangu, Ranchi ya Usangu, Ihefu, Madibila, Ubaruku na Kapunga, Januari 17, 2023. Ukaguzi huo unafuatia maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya marekebisho kwenye tangazo la Serikali namba 28 ambalo limetoa hekta 74,000 kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji endelevu. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo Kapunga, Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya ambapo aliwaeleza wananchi hao maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya marekebisho kwenye tangazo la Serikali namba 28 ambalo limetoa hekta 74,000 kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji endelevu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa eneo Kapunga, Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya, walimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kuhusu maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya marekebisho kwenye tangazo la Serikali namba 28 ambalo limetoa hekta 74,000 kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji endelevu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa baadhi ya maeneo ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji endelevu. Rais Dkt. Samia ameridhia kufanya marekebisho kwenye tangazo la Serikali namba 28 ambalo limetoa hekta 74,000 kwa ajili ya wananchi.
Share To:

Post A Comment: