Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi, Wananchi wa Pemba pamoja na Wanafunzi mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya mfano wa mlango unaopatikana Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Lela Muhammed Mussa mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Kwale mara baada ya ufunguzi wa shule hiyo leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya mavazi yanayovaliwa Kisiwani Pemba kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Lela Muhammed Mussa mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 09 Januari 2023 ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 9 Januari 2023 amefungua rasmi Skuli ya Msingi ya Kwale iliopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Ufunguzi wa Skuli hiyo ni miongoni mwa shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika kuelekea Sherehe za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Akihutubia mara baada ya ufunguzi wa Skuli hiyo, Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Nane ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuifanya sekta ya elimu kuwa sekta ya kipaumbele kwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za upungufu wa Madarasa na Walimu pamoja na kuzifanyia ukarabati skuli zote za zamani zilizopo Unguja na Pemba.

Aidha ameongeza kwamba Serikali imedhamiria kuajiri walimu wapya hasa wa masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuhakikisha kuwa inapunguza na kuondoa kabisa uhaba wa walimu Zanzibar.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imedhamiria kujenga miundombinu mingine muhimu kama vile maabara ya sayansi na kompyuta, maktaba pamoja na kuongeza idadi ya mabweni ili kuwawezesha watoto kupata muda mzuri wa kusoma.

Aidha Makamu wa Rais amesema tangu kipindi baada ya Mapinduzi matukufu, Serikali imeendelea kuongeza skuli katika Mikoa yote pamoja na kuboresha miundombinu ili kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora kwenye mazingira mazuri na salama. Ameongeza kwamba ni vyema kuhakikisha vijana wanarithishwa historia nzuri ya mapinduzi matukufu ili wafahamu umuhimu wa kuyaenzi na kuyalinda.

Amesema viongozi wakiongozwa na Hayati Mzee Abeid Amani Karume waliamua kufanya Mapinduzi ili kujikomboa na madhila ya kikoloni ambayo yalijaa unyanyasaji na ubaguzi mkubwa ikiwemo kupata elimu kiasi ambacho hata uhuru wa kujiletea maendeleo haukuwepo.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewasihi wazazi, walezi pamoja na wananchi wote kuhakikisha watoto wa kiume na wa kike wanaojiunga na skuli za msingi na sekondari wanamaliza masomo.

Amesema si vema kuwaruhusu watoto kukatisha masomo yao kwa sababu zisizo zozote zile.

Ametoa wito kwa hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa watakaobainika kufanya unyanyasi wa kijinsia na kingono, kuoa au kusababisha mimba za utotoni. Pia amesisitiza jamii kushirikiana kwa pamoja kulea watoto katika mila na desturi sahihi, maadili yaliyo mema na kushika mafundisho ya dini ambayo yatawaepusha na maovu mengi katika jamii inayowazunguka.

Makamu wa Rais amesema mifarakano katika familia, vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto pamoja na mmomonyoko wa maadili katika jamii vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto kutofikia malengo yao katika maisha.

Ametoa wito kwa kwa Watanzania wote kushirikiana kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kuchukua hatua pale ambapo watoto wananyimwa haki zao.

Aidha amesema ni muhimu Wizara husika kuhakikisha zinaimarisha Programu ya msaada wa ushauri wa Kisaikolojia kwa watoto, familia na jamii katika ngazi zote ili kupunguza athari na changamoto zinazotokea ndani ya familia na jamii zetu kwa ujumla.

Kwa Upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Lela Muhammed Mussa amesema jumla ya skuli mpya 45 zimejengwa Unguja na Pemba ndani ya mwaka mmoja katika hatua za kuimarisha sekta ya Elimu Zanzibar.

Waziri Lela amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi ni kuona Zanzibar inazidi kuboreka kielimu na hivyo mikakati madhubuti ya kuondoa wingi wa wanafunzi madarasani imewekwa ikiwemo kuandaa utaratibu wa kuondokana na mfumo wa wanafunzi kusoma kwa awamu mbili.

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Skuli hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Khamis Abdulla Said amesema jumla ya shilingi bilioni 2.5 zimetumika katika ujenzi wa skuli ikihusisha madarasa 21 na kuweza kuhudumia wanafunzi 1890 wanaosoma kwa wamu na hivyo kuondokana na changamoto ya mrundikano wa wanafunzi ilikuepo hapo awali.

Pia amesema Wizara ya Elimu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinashirikiana kwa karibu kuhakikisha changamoto katika sekta ya elimu zinaondolewa kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.

Katika Hafla ya Ufunguzi wa Skuli hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imependekeza Skuli hiyo kupewa jina la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.


Share To:

Post A Comment: