Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy amewataka makamishna wapya 47 wa uhifadhi kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ikiwemo kukabiliana na changamoto za uharibifu wa misitu.

Aidha amesisitiza mafunzo hayo ya uongozi  waliyoyapata yanaimarisha Jeshi ikiwemo utendaji kazi  wa kila siku ili kudhibiti matukio mbalimbali ya kulinda misitu ikiwemo kulinda amani ya nchi

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Uongozi wa Maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali, Mkeremy amesititiza uzalendo kwa wakala hao ili kutetea nchi na kulinda rasilimali zilizopo.

Amesema mafunzo hayo yalete mabadiliko ya utendaji kwa watumishi wenzao ikiwemo kubainisha masuala muhimu ya kufanyia kazi ili kuleta mabadiliko na ufanisi mahali pa kazi ikiwemo mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa mafunzo waliyopata kabla ya kupata uongozi.

"Kiongozi mzuri anapaswa kutatua changamoto zilizopo katika eneo hilo na bodi inatarajia kuona mabadiliko ya utendaji ikiwemo kujua elimu ya masuala ya kijeshi bado ni kubwa hivyo mafunzo ni muhimu ili kulinda uimara wa taasisi hiyo"

Niishukuru serikali kwakutoa rasilimali mbalimbali ikiwemo mafunzo ikiwemo kusimamia kidete ajenda ya uhifadhi kwakushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi ili yale yaliyoridhishwa yaendelee kuridhishwa na vizazi vingine vijavyo.

Miongoni mwa waliopata mafunzo hayo ni pamoja na makamishna 47 wa uhifadhi (TFS) ,wakiwemo mameneja  na wahifadhi wakuu  ambao kwa pamoja walipandishwa vyeo vipya

Ameishukuru menejimenti ya Bodi ya TFS kwa kufanikisha mafunzo hayo ya uongozi na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo na nufanisi katika utendaji wao wa kazi.

Makamishna hao awali walikuwa ni wahifadhi wasaidizi na hivi sasa wanakuwa wahifadhi waandamizi baada ya mabadaliko ya utendaji wa kitaasisi

Naye  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo aliwapongeza wakufunzi waliotoa mafunzo hayo ya kijeshi na alishukuru bodi hiyo ya TFS na maelekezo ya Mwenyekiti huyo Brigedia Jenerali Mkelami.

Amesema  asilimia 98 ya watumishi hao wameshapitia mafunzo ya kijeshi na mafunzo hayo ni awamu ya kwanza  kwa viongozi wa  yanayohusisha kada mbalimbali za rasilimali za misitu, uhifadhi wa rasilimali nyuki ikiwemo kukabiliana na changamoto za kiutendaji 

Ameongezea kwa kusema TFS inajumla ya misitu 463, wamashamba ya miti 24,hifadhi za mikoko,hifadhi misitu katika hifadhi asilia na usimamizi wa majukumu mbalimbali ngazi za serikali za mitaa huku akisema changamoto ya rasilimali hizo ni pamoja na uhaba wa watumishi,matukio ya moto katika maeneo ya misitu, uongezeko la matisho ya usalama kwa wananchi kujichukulia hatua pale yanapotokea matukio ya uvunaji haramu wa mbao na asali.

Pia ongezeko la matumizi ya kiteknolojia katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ambayo lazima elimu itolewe kwa wananchi katika kulinda mazingira 

Awali Akisoma  taarifa fupi ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi kwa maofisa hao jana katika Chuo cha Misitu Cha Olmotonyi,  Naibu Kamishna wa Uhifadhi (TFS)Huduma Saidizi,  Emmanuel  Wilfed alisema mafunzo hayo yalishirikisha  maofisa hao 47 na yalianza Januari 9 mwaka huu na kumalizia jana Januari 18 mwaka huu.

Pia makamishna hao walipata mafunzo ya uongozi,itifaki za kijeshi, oparesheni za kijeshi na na intalejensia mbalimbali.

Mafunzo hayo yameshirikisha makamishna kutoka makao makuu,makamanda wa uhifadhi kutoka maeneo mbalimbali,wahifadhi kutoka mashamba 23 kutoka mashamba ya uhifadhi na wahifadhi wa ufugaji nyuki.

 

Share To:

Post A Comment: