Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akizungumza mbele ya Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Januari 13,2023 katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam,pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally akifuatilia kwa makini.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya ameipongeza Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuandaa Mafunzo kwa Viongozi wa kamati ya Utekelezaji katika kuimarisha utendaji kazi.

Ametoa pongezi hizo Januari 13,2023 Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea eneo ambalo Mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwa viongozi wa Kamati ya Utekelezaji.

Aidha Bw.Maganya amewataka viongozi hao kuwa na upendo na kushirikiana katika kuijenga na kuiimarisha Jumuiya na kuondoa tofauti zao pindi zinapotokea

"Tukianza kukwaruzana kwaruzana,hatutakwenda,tushikamane, letu liwe moja na tuoneshe tofauti na Jumuiya zingine , utofauti uwe chanya usiwe utofauti wa kugongana gongana ,Kamati za utekelezaji mshikamane na uongozi wenu ufane". Amesema

Amesema Dar es Salaam lazima iendelee kubaki ya kuigwa kwa hivyo anashukuru kwa fursa hiyo wao hawajatengeneza baraza na wala hawana Kamati ya utekelezaji na kamati zingine ndogo ndogo kwasababu alitaka wapate muda kufahamiana vizuri pia .

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Taifa Bw. Fadhil Maganya ameipa heshima Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam kujipanga kwa pamoja katika maandalizi makubwa ya kuzindua kongamano la malezi la Jumuiya ya hiyo mapema mwaka huu, litakaloenda nchini nzima,na kwamba ameiomba mikoa mingine kuiga mfano wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanza mafunzo ya uongozi kwa uharaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally amesema dhumuni la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanatengeneza viongozi sahihi katika nyakati sahihi ili waweze kuongoza Jumuiya na Chama cha Mapinduzi nchini.

Pamoja na hayo Bi.Khadija amesema kuwa katika kuelekea kwenye Uchaguzi 2024 pamoja na 2025 dhumuni la Jumuiya na Chama kwa ujumla ni kuhakikisha wanapata ushindi kwa kishindo.

"Ushindi wa kishindo ambao tunaenda kuupata lazima tuwe na viongozi makini ambao wanakisi sifa na weledi katika Chama cha mapinduzi kwahiyo wametekeleza azimio la Mkutano Mkuu wa Kumi kwa kutoa Mafunzo kwa vitendo na tumeanza na Mkoa wa Dar es Salaam". Amesema

Hata hivyo amemuhakikishia Mwenyekiti kwamba Mkoa wa Dar es Salaam uko tayari kushirikiana nae bega kwa bega na kuhakikisha dira yake ya Jumuiya ya Wazazi inang'ara na kuisimamia vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Mkoa huo na taifa kwa Ujumla.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akifafanua jambo mbele ya Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Januari 13,2023 katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam,pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally akifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akimshukuru Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally kwa kuandaa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam  katika kujiimarisha zaidi kwenye suala la Uongozi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akiteta jambo Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally wakati wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Ally akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya alipotembelea kambi ya mafunzo hayo ya siku tatu kwa Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yanayoendelea katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Mafunzo wakiendelea kusikiliza yaliyokuwa yakijiri

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa mafunzo pamoja na Wakufunzi wa Mafunzo hayo.
Share To:

Post A Comment: