Azam FC wameshindwa kufuzu hatua ya Fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2023 baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya timu ya Singida Big Stars kwenye uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.

Singida BS wamefuzu hatua ya Fainali ya mashindano hayo kwa mabao yao yaliyofunywa na Mshambuliaji Kazadi Kasengu kwenye dakika za 27’ 53’ 64’ na 86’ wakati ba la Azam FC lilifungwa na Mshambuliaji Abdul Suleiman Sopu kwenye dakika ya 43’ ya mchezo.

Singida BS wamefuzu kucheza Fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza, na watasubiri mshindi kati ya Mlandege dhidi ya Namungo FC katika Nusu Fainali ya pili itakayochezwa Januari 9, 2023 kwenye uwanja huo huo wa Amaan visiwani humo.

Fainali ya mashindano ya Mapinduzi itachezwa, Januari 13, 2023 kwenye uwanja wa Amaan ikiwa ni siku moja tu baada ya maadhimisho ya sherehe za miaka 59 za Mapinduzi ya Zanzibar.

Share To:

Post A Comment: