Angela Msimbira ARUSHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amewaagiza Maafisa elimu Maalum wote nchini kuhakikisha wanasimamia zoezi la uchunguzi wa awali wa watoto ili kubaini watoto wenye mahitaji maalum katika jamii.

Ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba, 2022 wakati akifungua  mafunzo kwa maafisa elimu watu Wazima na maafisa elimu Maalum  iliyofanyika  katika ukumbi wa chuo cha Ualimu Patandi, Mkoani Arusha.

Amewataka kuhakikisha wanatumia vituo vya uchunguzi (Education Support Resource Assessment Centre) na kuwaelekeza watoto wenye mahitaji maalum katika shule stahiki ambazo wanapaswa kupelekwa ili wapate afua stahiki

Waziri Kairuki ameelekeza shughuli za usimamizi na uendeshaji wa elimu zihusishe  kikamilifu  masuala ya elimu maalumu  na elimu ya watu wazima kwa kuhakikisha wanashirikiana  na viongozi katika jamii katika kuratibu  shughuli za elimu ya watu wazima na elimu Maalum katika shule za msingi  na Sekondari

Ametoa rai kwa Maafisa hao kuweka utaratibu wa kupokea wanafunzi wenye mahitaji maalum  wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali kwa mwaka 2023 kwa kushirikiana  na viongozi katika maeneo yao ili kuweka mazingira bora kwa wanafunzi hao

Waziri Kaituki amewataka viongozi wa elimu  katika ngazi ya shule, Kata, Halmashauri na Mikoa kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji shuleni na kushirikiana na walimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata umahiri uliokusudiwa badala ya kukaa ofisini.

Aidha,ameagiza kila mwalimu lijiwekea  malengo binafsi katika masomo anayofundisha na kuhakikisha hakuna mwanafunzi  anayeshindwa  kupata umahiri uliokusudiwa  katika somo lake ifikapo mwishoni mwa kila mwaka




Share To:

Post A Comment: