Jumla ya wasimamizi 248 wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Njombe mjini unaotarajiwa kufanyika Disemba 17 mwaka huu wamekula kiapo cha kwenda kusimamia uchaguzi huo kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi. 


Wakati wa mafunzo kwa wasimamizi hao katika halmashauri ya mji wa Njombe mratibu wa uchaguzi jimbo la Njombe mjini Kenani Maliga amesema mafunzo hayo yanalenga kuwaelekeza sheria na kanuni zote za kusimamia uchaguzi huo pamoja na taratibu zake. 


Mkurugenzi wa uchaguzi huo Kuruthum Sadick ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe anawataka wasimamizi hao kwenda kutekeleza kiapo chao na sio kwenda kinyume cha sheria. 


Mwenyekiti wa mafunzo hayo Jimy Ngumbuke yeye anasema hawatoiangusha tume ya uchaguzi katika uchaguzi huo. 


Nuru Baptist na Timotheo Mtewele ni baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi huo waliokula kiapo ambao wanakiri kwenda kuhakikishia zoezi hilo linafanyika kwa weledi mkubwa kwa kadri ya kiapo chao. 


Uchaguzi huo mdogo unakwenda kufanyika baada ya kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Romanus Mayemba ambaye alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe aliyefariki octoba 23 mwaka 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Share To:

Post A Comment: