Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu  akiongoza kikao cha kamati ya mfuko wa Jimbo kilichoketi jana Disemba 22, 2022 jimboni humo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga.

Na Dotto Mwaibale, Singida 

ZAIDI ya Sh.67 Milioni zimeelekezwa kuchagiza na kuchochea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Singida Mashariki.

Akizungumza Disemba 22,2022 wakati akiongoza kikao cha kamati ya mfuko wa Jimbo, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu alisema fedha hizo zinakwenda kutekeleza miradi mbalimbali kwenye jimbo hilo na akaomba zikatumike kukamilisha miradi yenye viwango na thamani halisi ya fedha hizo.

 Katika hatua nyingine   Taasisi ya Tanzania Youth  Elite Community (TYEC) kwa kuutambua  uzalendo  halisi wa nchi imemtunuku tuzo ya heshima mbunge huyo ikiwa ni kutambua juhudi zake katika kuchagiza maendeleo ya wananchi jimboni humo.

Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo Shigela Denis alisema wameamua kumtunuku tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa anaoufanya wa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

"Mbunge Mtaturu amekuwa ni chachu kubwa ya maendeleo katika jimbo la Singida Mashariki na kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa katika jimbo hilo amefanya mambo makubwa na kwa kulitambua hilo kupitia taasisi yetu tumeamua kumtunuku tuzo hii ya heshima" alisema Shigela,

Akizungumza baada ya kutunukiwa tuzo hiyo aliishukuru taasisi kwa kutambua mchango wake na kueleza  tuzo hiyo ni ya Heshima kwa wananchi wote wa Wilaya ya Ikungi na si peke yake.

Katibu Mtendaji wa  Taasisi ya Tanzania Youth  Elite Community (TYEC)  Shigela  Denis akimkabidhi tuzo ya heshima (cheti) Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa wa maendeleo katika jimbo hilo.


Picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo.
Kikao cha kamati ya mfuko wa jimbo kikiendelea.
Mjumbe wa kamati ya mfuko wa jimbo hilo, Yahaya Njiku akichangia jambo kwenye kikao hicho. 
Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: