Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Mgalo iliyopo mkoani Iringa Carister Haule(15)mkazi wa kijiji cha Lifua wilayani Ludewa mkoa wa Njombe amefariki dunia kwa kupigwa na radi wakati akifungulia mbuzi chini ya mti,pamoja na nyumba16 kuezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali.


Kaimu katibu tawala  ya wilaya ya Ludewa Daniel Ngalupela,alisema tukio hilo limetokea disemba 17 majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Lifua kata ya Luilo.

"Madhara makubwa yaliyojitokeza ni kifo huyo binti mwanafunzi  kidato cha pili amepigwa radi akiwa anafungulia mbuzi waliokua amefungwa kwenye mti mkubwa wa mkorosho,radi imeleta madhara ya kifo cha mwanafunzi pamoja na hao mbuzi"alisema Ngalupela.

Hata hivyo Ngalupela alisema kuwa kati ya nyumba 16,nyumba sita zimebomoka kabisa.

"Kitu cha kwanza kama wilaya tumefanya tathimini ya athari zilizojitokeza baada ya hapo kukutana na wadau kwa ajili ya kuwachangia ili kuwasaidia kupata vifaa kama mabati,mbao ili kuweza kuzirudisha hizo nyumba katika hali ya kawaida"alisema Ngalupela.

Alisema jitihada ya dharura ambayo imechukuliwa ni pamoja na kuwaomba baadhi ya wananchi kuwahifadhi watu ambao wamepata madhara.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Allen Ngatunga alisema aliwasiwasili katika eneo la tukio na kumkuta binti huyo akiwa amelala chini pamoja na mbuzi hao.



Share To:

Post A Comment: