Angela Msimbira  - ARUSHA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki  amesema hatasita kuwachukulia hatua stahiki kwa  wale wote watakaovuruga, kufuja fedha za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Shule za Awali na Msingi kwenye utekelezaji wa Mr Sekondari adi wa Uboreshaji wa Elimu ya  Awali na Msingi (BOOST)  

 

Ameyasema hayo leo tarehe 13 Disemba, 2022 wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa timu za utekelezaji wa mradi wa BOOST  katika Mikoa ya Singida, Manyara na Arusha, uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Ilboru mkoani Arusha. 

“Serikali inapimwa kwa vigezo katika kutekeleza Mradi wa BOOST nchini sitakuwa tayari  kuona fedha  zimetolewa kiasi cha shilingi trilioni 1.15 na kupelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa lakini miradi haitekelezwi kwa wakati na fedha hizo kurudishwa, tutakuwa hatujatenda haki kwa wananchi” amesisitiza Waziri Kairuki


Waziri Kairuki amewataka Wajumbe wa mradi huo kuhakikisha fedha zinazotolewa katika utekelezaji wa miradi zinakamilisha miradi iliyopangwa ili kuepusha miradi mingi kutokukamilika huku fedha zikiwa zimekwisha .

Amewataka wajumbe hao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano na jamii katika utekelezaji wa mradi na kutekeleza afua zote za mradi kwa wakati ukiwemo ujenzi wa miundombinu ili kufikia matokeo yaliyokubalika; 


Aidha, amewaagiza Wajumbe hao kuwahamasisha wazazi/walezi kuwapeleka watoto wenye umri wa kuanza shule ili waandikishwe na kuanza shule kwa wakati ili  kuwaepushia  mzigo walimu wa kulazimika kurudia kufundisha mambo yale yale kutokana na wanafunzi wengine kucheleweshwa kuanza shule.


Share To:

Post A Comment: