Na : Joel Maduka Geita

Wafanyabiashara Wilayani Bukombe Mkoani Geita wametakiwa kuzingatia utunzaji wa kumbukumbu za biashara likiwemo suala la  risiti za manunuzi, mauzo na gharama za biashara lengo likiwa ni  kulipa kodi stahiki na pia kutekeleza matakwa ya kisheria.

Hayo yamesemwa na afisa elimu na huduma kwa Mlipa kodi ,Justine Katiti wakati wa semina ambayo imetolewa na  Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Geita.Ambayo ilikuwa imelenga kuwaelekeza wafanyabiashara namna bora ya kutunza Kumbu kumbu za kibiashara.

Bw.Katiti  amesema wafanyabiashara wamekuwa na mwitikio mdogo wa kutoa risiti kwenye mauzo ya bidhaa na huduma lakini pia wanunuzi nao kutodai risiti kwenye manunuzi wanayofanya na hivyo kuikosesha Serikali kukusanya mapato.

Aidha ameongeza kuwa  adhabu kali zinatolewa kwa mujibu wa sheria dhidi ya Wafanyabiashara wasiotoa risiti ambapo adhabu yake ni kuanzia Tshs Milioni .3. hadi Tshs Milioni .4.5  na pia mnunuzi asipodai risiti adhabu yake ni kuanzia Tshs.30,000 hadi Tshs Milioni.1.5.

Katika semina hiyo Wafanyabiashara walitahadharishwa kujiepusha na watu ambao ni matapeli wanaojifanya ni Maafisa wa TRA na kwamba inapotokea wana mashaka na watu hao, watoe taarifa mapema kwenye ofisi ya TRA iliyo karibu nao.

Kwa upande wa Wafanyabiashara waliishukuru TRA kwa kuandaa semina hiyo na kuomba semina ziwe zinafanyika mara kwa mara ili kukumbushana mambo mbalimbali ya kodi.




Share To:

Post A Comment: