Serikali imewataka Watanzania kutokudharau tetesi yeyote watakayosikia juu ya uwepo wa mtu unayedhani ana dalili za  ugonjwa wa Ebola kufuatia ugonjwa huo kuua zaidi ya watu 130 nchini Uganda.Katika Taarifa yake wakati akizindua mafunzo ya kuitambua,kujikinga na kumhudumia mgonjwa wa Ebola yakichua siku nne Kwa watumishi wa Afya Kwa Halimashuri zote za Mkoa wa Dar es Salaam waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali imechua hatua hiyo kufuatia watumishi wengi wa Afya kufarik wakati wakihudumia wagonjwa

Hata hivyo mafunzo hayo pia yamehusisha wataalamu kutoka shirika la afya Duniani WHO Ili kuwakumbusha ipi ni miongozo ya magonjwa ya mlipuko

Akieleza Hali ilivyo Kwa Mkoa wa Dar es Salaam Mganga mkuu Dkt Rashid Mfaume amesema kufuatia mwingiliano wa kibiashara kuwa mkubwa  wameamua sasa kiyadhibiti maeneo ya uwanja wa ndege,bandarini Kwa kuwa ni rahisi watu kutoka nchi jirani na kuingia hivyo kupitia mafunzo Kwa watumishi itasaidia zaidi.

Imeelezwa kuwa Asilimia 80 ya Huduma za Afya hutolewa na vituo vya afya ama poly kliniki za watu binafsi katika Mkoa wa Dar es Salaam hivyo ndo maana serikali imewajumuisha katika mafunzo Ili kupata utambuzi Kwa kuwa wagonjwa wengi huanzia  vituoni kwao

Share To:

Post A Comment: