DENIS CHAMBI, TANGA.

Mkoa wa Tanga umetenga zaidi ya hekali zipatazo 300 kwaajili ya ujenzi wa viwanja vya michezo mbalimbali katika wilaya ya Mkinga hii ikiwa ni hatua ya kuzidi kuongeza hamasa ya michezo kwa jamii pamoja na kuibua  vijana wenye vipaji kwa wingi zaidi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati akifungua michuano ya Crdb taifa  Cup inayoalshindanisha timu 36 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara katika mchezo wa Kikapu inayofanyika kitaifa mkoani Tanga.

Mgumba alisema kuwa dhamira ya serikali ni njema sana katika sekta ya michezo kwani imeendelea kuwekeza na kuboresha miundombinu ikiwa inatarajia kuona michezo yote inainuka kote nchini vijana na wanamichezo kwa ujumla wanapata maendeleo endelevu.

"Mafaniko ya sekta ya michezo hapa nchini kwa sehemu kubwa yanajumuisha mchango wa wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwepo bank ya kizalendo ya Crdb binafsi nafurahia na kuwapongeza kwa kuweka uwekezaji mkubwa  katika mpira huu wa Kikapu na kutoa udhamini kwa mwaka wa tatu mfululizo kwa ligi  ya Taifa"

"Sisi mkoa wa Tanga  hatuko nyuma katika maendeleo ya michezo hapa nchini na sisi tumejipanga vizuri tumeshatenga eneo zaidi ya hekali mia tatu kule  Mkinga kwaajili ya kuanzisha Kijiji maalumu cha michezo kwa michezo yote inayochezwa hapa nchini itapatikana , dhamira yetu ni kujenga viwanja vitano vya kila aina ya mchezo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tanga. " alisema

Michuano hiyo ambayo inaendelea  kurindima katika viwanja viwili vya Habours klabu pamoja na Mkwakwani  imeanza   November 4 timu zote zikichuana kumtafuta bingwa wa mwaka 2022 kwa upande wa Wanaume na wanawake kila mmoja  bingwa akijishindia  kitita cha shilingi Million 10 huku mshindi wa pili akisepa na million tano zawadi ambazo zimenogeshwa na mdhamini wa ligi hiyo banki ya CRDB.

Crdb imezidi kuongeza hamasa kwa wachezaji na vijana wengi kupenda mchezo huo kwani zaidi ya vijana 40  kupitia mpira wa Kikapu wamekuwa wakipata ufadhili wa kimasomo  huku wengine wakipata kazi za kujiingizia kipato katika maeneo mabalimbali hapa nchini.

Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa alisema kuwa  dhamira yao ni kuona mchezo huo unazidi kukua hapa nchini ambao utaendana sambamba na maendeleo ya vijana wanaochezea mchezo huo hatua ambayo itakwenda kupunguza wimbi la vijana nchini wasio na kazi za kudumu ambapo wengi wao wamekuwa wakijiingiza katika makundi hatarishi

"Moja kati ya malengo ya  Crdb Taifa Cup ni kuleta hamasa ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaocheza  katika mikoa yote hapa nchini,

Alisema kuwa mbali na mchango wanaoutoa kupitia michezo wamekuwa ni wadua wakubwa wa maendeleo pia ambapo kwa kipindi cha mwaka jana benk hiyo iliweza kutoa shilingi Million 10 kwaajili ya vifaa vya ujenzi wa shule nne zilizopo wilaya ya Kilindi mkoani hapa, wakitoa pia million 40 kwaajili ya ujenzi wa  madarasa na ofisi ya walimu katika shule maalumu  Chuda iliyopo jijini Tanga.

Sisi Crdb ni wadau wakubwa wa maendeleo mkoani Tanga na hata kanda nzima ya Kaskazini kwa ujumla wake ,  hapa Tanga kwa mwaka jana  benki ilitoa vifaa vya ujenzi kwaali ya ujenzi wa shule iliyopo Kilindi  vyenye thamani ya shilingi Million 10 kama moja ya muendelezo wa mipango ya benki  katika sera yake ya kuwekeza katika jamii, pia  benki ilitoa million arobaini kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu katika shule maalumu ya Chuda ambayo yatakwenda kuzinduliwa mwaka huu", alisema Chiku.

"Vilevile mwaka 2022 tulitoa ufadhili wa taulo za kike  kwa wanafunzi wa shule za msingi za wilaya ya Tanga mjini hii inaendana kabisa na ajenda yetu  ya kuwezesha vijana kufikia ndoto zao Kama moja ya vipaumbele ya benki ya Crdb" aliongeza.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania

Rwehabura Barongo kadiri siku zinavyokwenda maendeleo ya mpira wa Kikapu yanazidi kuonekana na kuleta Mapinduzi makubwa kwa maendeleo ya wachezaji na Chama hicho hatua ambayo inachagizwa kwa kiasi kikubwa na wadau mabalimbali wanaojitoa katika kusaidia mchezo huo wakiwemo wadhamini wakubwa wa ligi hiyo ngazi ya Taifa  benki ya Crdb.

"Sasa hivi Tanzania hii huwezi kuzungumzia  basketball bila kutaja benki ya Crdb na hii fursa imekuwa sio ya wadau wa Tanzania pekee bali hata kimataifa ,  tumepata barua kutoka  Giant of  Afrika wataleta skauti wao kuja  kuangalia vipaji vya mpira wa Kikapu Tanzania  haya ni kutokana na  matokeo chanya ya ushirikiano wa mikoa yote  inayoshiriki ambao walikuwa na ligi za mkoa walizofanya kwa wakati na muda sahihi" alisema Barongo.

Uzinduzi wa ligi hiyo amabao umefanyika juzi November 4 itaendelea hadi November 12 ikiwa ni rara ya kwanza kufanyika mkoani Tanga na mara ya tatu kuchezwa kwa ligi hiyo hapa nchini ikifanyika kwa Mara mbili mfululizo mkoani Dodoma bingwa kwa upande wa wanawake  Wanaume akitarajiwa kuondoka na  kitita cha shilingi million 10, huku washindi wa pili wqo wakijinyakulia  shilingi million 5 uwwkezaji ambao  mkubwa ambao umefanywa na benki ya Crdb.

Share To:

Post A Comment: