Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la polisi limefanikiwa kukamata vifaaa mbalimbali vya vilivyoibwa kwenye miundombinu ya umeme katika mradi wa reli ya mwendokasi.


Zoezi hilo maalumu la kulinda na kuhakikisha nyara za serikali zinaendelea kuwa salama linaloendeshwa na Serikali kupitia TANESCO na Jeshi la polisi limezaa matunda baada ya kukamatwa kwa baadhi ya vifaa vya umeme vinavyotumika katika reli ya mwendokasi ambavyo viliibiwa na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni.


Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt Mussa Ali akizungumza na Waandishi wa habari amesema zoezi hilo maalumu la kulinda nyara za Seriakli limeleta matokeo chanya ndani ya muda mfupi na kwamba litakuwa endelevu na kuhakikisha wale wote wanaohusika na wizi wa mindombinu ya shirika hilo watakapotiwa nguvuni.


Kwa upande wake Meneja usalama wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Lenin Kiobya akatoa rai kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu kuzingatia uhalali wa vyuma wanavyoletewa kwa ajili ya kununua na baadaye kuviuza.

Share To:

Post A Comment: