Makala ya Royal Tour imeendelea kuleta mapinduzi katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Utalii pamoja na sekta nyingine kutokana na nafasi inazoendelea kuzalisha kama vile mikutano mikubwa ya kimataifa ambayo imeendelea kufanyika nchini na kuifanya Tanzania kuendelea kufanya vyema katika kuvutia watalii na wawekezaji wa sekta tofauti tofauti.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt.Hassani Abbas wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 4,2022 Jijini Dar es Salaam

Amesema moja ya fursa zilizoletwa na Makala ya Royal Tour ni Tamasha la Kimataifa la Wadau wa Tasnia ya Muziki Duniani lijulikanalo kama Acces Music ambalo linatafajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Novemba 24 hadi 26 mwaka huu na kuhusisha mataifa mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Marekani na Afrika ambapo licha ya kusaidia kuinua wasanii nchini pia inategemewa kukuza sekta mbalimbali..

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Muziki Afrika Eddie Hatitye ambao ndio waandaaji wa matamasha hayo ya Acces amesema Tanzania inakuwa nchi ya tano barani Afrika kuandaa Tamasha hilo linalokutanisha wadau wa sekta ya muziki kutoka makampuni na wadau binafsi ambao wamekuwa na mchango katika kuinua sekta ya sanaa ya muziki.

Naye Katibu wa Shirikisho la Muziki nchini Farid Kubanda akizungumza kwa niaba ya wana muziki wa Kitanzania amesema hiyo ni nafasi muhimu katika kukuza uelewa na namna ya kuendesha sekta ya muziki kama biashara jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: