Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (katikati) akifanya tukio la ufunguzi wa jengo jipya la la Maabara na Ofisi, Kituo cha Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kinachohudumia wafugaji wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa TVLA Dkt. Stella Bitanyi na kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi wa muonekano mpya wa Tovuti ya Wakala (www.tvla.go.tz) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kuhusiana na maabara mpya ya Kituo cha Iringa itakavyofanya kazi mara baada ya kufunguliwa Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo. Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (Katikati waliokaa), Watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) na viongozi wa Mkoa wa Iringa walipokuja kwenye halfa fupi ya kuhitimishwa kwa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa.

**********************

◼️ Yahamasisha uanzishwaji wa Wiki ya Mifugo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda ameipongeza Waakala ya Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) kwa ubunifu wa kuadhimisha wiki maalum ya wakala hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwake ambapo kufuatia kufana kwa Maadhimisho hayo Nzunda amemuagiza Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini Prof. Hezron Nonga kuweka utaratibu wa kuanzisha wiki ya Mifugo kuanzia mwaka ujao wa fedha ambayo itazishirikisha Taasisi zote za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo pamoja na zile zilizopo Sekretariati za Mikoa, mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau kutoka Sekta binafsi.

Nzunda ametoa pongezi hizo kwenye kilele cha Maadhimisho hayo kilichofanyika Novemba 25,2022 mkoani Iringa ambapo hafla hiyo pia iliambatana na Ufunguzi wa jengo jipya la kituo cha Wakala hiyo kilichopo eneo la Isoka Machinjioni mkoani humo kinachotarajiwa kuhudumia wafugaji wote waliopo kanda ya nyanda za juu kusini.

“Ubunifu huu ndio mtazamo wa Wizara kwa sasa na kwa kufanya hivi sio tu tumeweza kutangaza shughuli za Taasisi bali tumefanikiwa kuelimisha umma na kufanya mawasiliano ya karibu na jamii tunayoihudumia kupitia vyombo vya habari, vikundi mbalimbali na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Tovuti ya Wakala na ninaamini Taasisi nyingine zilizopo chini ya Wizara zitaiga jambo hili” Ameongeza Nzunda.

Akizungumzia jengo jipya la Wakala hiyo alilolizindua Nzunda amewataka viongozi wa Mkoa wa Iringa kuwahamasisha wananchi na wafugaji wote mkoani humo kutumia huduma zinazotolewa kituoni hapo ili waweze kuboresha mifugo yao na kukuza uchumi wa mfugaji mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Huu ni wakati wa kufuga kisayansi na ndio maana tumewaletea kituo hiki ili kiwasaidie kutekeleza shughuli zenu za ufugaji kisasa zaidi na kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia yaliyopo ulimwenguni kote hasa kupitia mfumo mpya wa kidijitali wa kusajili viuatilifu vya mifugo, ufuatiliaji, uzalishaji na usambazaji wa chanjo unaotumiwa na TVLA kwa sasa na kwa hili niwapongeze sana kwani mtapunguza upotevu wa mapato na kurahisisha sana utendaji wenu” Amesema Nzunda.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Stella Bitanyi amesema kuwa katika kipindi cha Wiki moja ya Maadhimisho hayo, Wakala hiyo imefanikiwa kutoa bure dozi 150,000 za chanjo ya magonjwa ya Kimeta, Mdondo, Homa ya mapafu ya Mbuzi/Ng’ombe, Chambavu na Kutupa mimba zenye thamani ya zaidi ya Tshs.Mil.5 Kutembelea viwanda 50 vinavyozalisha vyakula vya Mifugo ili kutoa elimu ya uhakiki wa ubora wa vyakula vinavyozalishwa, kuhamasisha wananchi juu ya matumizi ya huduma na bidhaa zinazotolewa na Wakala hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutembelea na kutoa misaada kwa wasiojiweza na kwenye vituo 7 vya Watoto yatima vilivyopo maeneo mbalimbali hapa nchini, kufanya uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya mifugo bure kwenye sampuli 400 za wanyama mbalimbali katika maabara za Wakala, kutoa huduma za uogeshaji bure kwa Mbwa 200 na kuwahamasisha wananchi kutumia huduma ya usajili na uchambuzi wa ubora wa viuatilifu vya Mifugo ambayo sasa inatolewa na Wakala hiyo kupitia vituo vyake vyote nchini.

“Sambamba na hayo Wakala katika kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha miaka 10 tunajivunia mafanikio tuliyopata katika kutoa huduma na bidhaa za kiveterinari hapa nchini na miongoni mwake ni pamoja na Kuongezeka vituo 2 vya maabara kutoka vituo 11 mwaka 2012 hadi 13 mwaka 2022, Kupatikana kwa Ithibati (accreditation) katika uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya mifugo kulingana na kanuni za kimataifa, kuongeza mapato ya ndani kutoka milioni 220 hadi bilioni 3.1 kwa mwaka 2022, na kujengea uwezo maabara ya kupima ubora wa vyakula vya mifugo, kuangamiza Mbung’o wanaoeneza ugonjwa wa Nagana kwa Ng’ombe na Malale kwa binadamu pamoja na Kupewa jukumu jipya la kusajili na kuthibitisha ubora wa viuatilifu vya mifugo kuanzia mwezi Julai 2022” Ameongeza Dkt. Bitanyi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Elias Luvanda mbali na kuishukuru Wizara kwa kuamua kujenga Kituo cha Wakala hiyo mkoani kwake, amesema kuwa kituo hicho kimejengwa mahali sahihi kwani mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya Mifugo ambapo mpaka sasa una takribani mifugo Mil. 8.7 ambayo inajumuisha Ngombe Mbuzi, Kondoo, Nguruwe, Punda, Kuku, Mbwa na Paka.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa ambako ndipo kilipojengwa kituo hicho Mhe. Ibrahim Ngwada alisema kuwa Halmashauri yake itaendelea kuweka mazingira Wezeshi kwa Serikali kutekeleza miradi yake ambapo ameahidi kufikisha kwenye vikao vyao vya kisheria suala la lililokuwa eneo la Wakala ya Maabara ya Veterinari nchini lililochukuliwa na Halmashauri hiyo ili lirejeshwe kwa wakala hiyo jambo ambalo litaiwezesha kupanua wigo wa huduma zake.

Akiongea kwa niaba ya wafugaji, mwakilishi wa Mkurugenzi wa ASAS LTD Dkt. Isaya Keto amesema kuwa wao kama sekta binafsi wanajivunia uwepo wa Wakala hiyo nchini ambapo ameishukuru kwa ushirikiano wanaotoa kwa wafugaji huku akisisitiza wafugaji wenzake wote nchini kutumia chanjo zinazozalishwa na wakala hiyo kutokana na ubora wa chanjo zake..

Maadhimisho ya Wiki ya Wakala ya Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Tambua, Tibu na Dhibiti Magonjwa ya Mifugo” na yalianza rasmi Novemba 21-25 mwaka huu.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: