Mwenyekiti wa michezo kutoka Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifuTPHPA Mohammed Mpina.

Na Denis Chambi, Tanga.

Mwalimu mwenye taaluma ya leseni A ya ukocha wa mpira wa miguu Mohammed Laizer kutoka mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu iliyopo mkoani Arusha 'TPHPA' amewaomba waajiri wa taasisi zilizopo hapa nchini kutoa muda wa kutosha kwaajili ya kuandaa timu zinazokwenda kuwawakilisha katika michezo mbalimbali hapa nchini ili waweze kiwa na vikosi bora vitakavyosaidia kufikia malengo ya kufanya vizuri.

 Laizer ametoa ombi hilo mkoani Tanga wakati akishiriki mashindano yanayohusisha watumishi mashirika ya umma, taasisi binafi na makampuni almaarufu kama 'SHIMUTA' kwa michezo mbalimbali kushindaniwa ambapo amesema timu nyingi zinashindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa muda mrefu wa kufanya maandalizi kwa pamoja.

 "Kwa uhalisia Tanzania ina vipaji vingi sana kila mashindano yakapokwenda kufanyika lazima utaona vipaji isipokuwa tatizo ni kwamba wengi wanaoshiriki haya mashindano ni watu wazima na watumishi kwahiyo huwezi kumtoa na kumpelekea kwenye klabu yeyote kuanzia ligi ya wilaya"

 "Taasisi nyingi kama bado mwezi mmoja kwenda kwenye mashindano ndio unapewa timu kuiandaa, wakati unapewa wengi wanakuwa sio wazoefu katika michezo na wengi wao ni watumishi kwahiyo wanahitaji kupewa muda mrefu wa kufanya mazoezi" alisema Laizer.

 Katika mchezo wao wa mwisho kwenye makundi waliocheza timu hiyo ya TPHPA imeingi kibabe kwenye hatua ya 16 bora baada ya kuitembezea kichapo cha mabao 4-0 timu kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya 'NHIF'. 

 Akizungumza mwenyekiti wa michezo kutoka TPHPA Mohammed Mpina amesema kuwa timu zao kushiriki ligi ya kanda ya kaskazini imekuwa na matokeo chanya kwenye mashindano ya shimuta mwaka huu yanayoendelea mkoani Tanga huku wakiamini kuwa wanakwenda kuweka rekodi mpya.

 "Siri ya kufanya vizuri kwenye hatua hii ya makundi imetokana na maandalizi kanda ya kaskazini tuliandaa ligi yetu ya timu za Shimuta ambayo tumekuwa tukifanya vizuri lakini kumekuwa na muunganiko mzuri kati ya TPRI na PHS kwahiyo kwa muunganiko huu tumeweza kupata wachezaji wa ziada ambao wamekuja kuboresha timu yetu", 

 "Mashindano ya mwaka huu yana ushindani mkubwa cha msingi ni kuandaa timu hapa tulipofikia ni mafanikio makubwa kwa sababu mara yetu ya kwanza kushiriki Shimuta ilikiwa 2019 timu yetu ya mpira wa miguu haikuweza kushinda hata mchezo mmoja na kiwango cha chini kufungwa ilikuwa ni magoli saba kwahiyo utaona ni jinsi gani timu yetu imekuwa ikikuwa mwaka hadi mwaka" 

 Kwa upande wake mwenyekiti wa michezo kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF Sifu Tenjela amelia na majeruhi wengi pamoja na wachezaji wao kushindwa kuwa pamoja kwa muda mrefu kwenye timu yao ambao ndio sababu ya wao kushindwa kufanya vizuri kunako mashindano hayo.
Share To:

Post A Comment: