Mkuu wa idara ya michezo na burudani kutoka chuo hicho cha Mocu , Hossein Laizer .

Na Denis Chambi, Tanga.

Licha ya kutupwa nje ya mashindano ya Shimuta yanayoendelea mkoani Tanga chuo kikuu cha ushirika Moshi 'Mocu' wamelipongeza shirikisho linalisimamia michezo hiyo huku wakiiomba kuendelea kudhibiti mamluki ambao kimsingi sio walengwa wa mashindano hayo ili yaweze kuleta tija na manufaa yaliyolengwa kwa watumishj kutoka mashirika ya umma taasisi na makampuni hapa nchini.

 Chuo cha Ushirika Moshi 'Mocu' ambao walikuwa na malengo ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ndoto zao zimeishia njiani na kugonga mwamba kwenye mpira wa miguu baada ya kupoteza mechi zote walizoshiriki hatua ya makundi huku wenzao timu za kutoka mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' pamoja na KCMC waliokuwa nao kwenye kundi moja wakifanikiwa kusonga mbele na kuingia hatua ya 16 bora. 

 Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa idara ya michezo na burudani kutoka chuo hicho cha Mocu , Hossein Laizer  amesema kuwa hawanabudi kuwapongeza shirikisho la michezo hiyo Shimuta kwa namna wanavyoboresha ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa mamluki na kuiomba kwa mwakani kuongez kasi ya ukaguzi.

 "Nawapongeza sana Shimuta kwa zile hatua wanazoenda kufanya kushugulikia suala zima la mamluki , shirikisho linajitahidi sana lakini tunajua udanganyifu hua lazima upo niendelee kuwaomba hata mwakani waendelee kufanya ukaguzi ikiwezekana waweze kuzishirikisha hata zile taasisi ambazo zinahusika katika kuhakikisha kwamba wanaoshiriki michezo hii ni watumishi kweli"

 "Ukiangalia tulikotoka na hapa tulipo shirikisho wamejitahidi sana kushugulikia suala la mamluki ninawashukuru na kuwapongeza sana kwahiyo mimi niwaombe waendelee kushugulikia changamamoto hii kwa sababu lengo kubwa la michezo hii ni kuhimiza mazoezi mahala pa kazi ili michezo iweze kuwa na tija na watumiahi wetu waweze kuboresha afya zao" aliongeza. 

 Hassan amekiri uwepo wa ugumu wa michezo hiyo hii ni kutokana na ushindani waliokutana nao kwa timu pinzani kila mmoja akionyesha kujipanga kwa namna yake akiyapania mashindano hayo ili kuhakikisha harudi mikono mitupu. 

 "Mpira ni mchezo wa makosa, katika upande wa timu yetu kuna makosa tumeyafanya na yameenda kutuadhibu lakini kwa hatua tuliyofikia tumeona mapungufu yakowapi sasa tupo katika hatua ya kutengeneza timu yetu tunaenda kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza na tunaahidi kwa mwaka ujao tunaweza kupiga hatua mbele zaidi" alisema.

 Aliwapongeza viongozi wao kutoka Mocu kwa namna walivyofanya maandalizi kuhakikisha taasisi yao inakwenda kushiriki shimuta kikamilifu licha ya kushindwa kutimiza matarajio yao kwa mwaka huu kunako michezo hiyo lakini amewaahidi kwenda kusimamia na kujipanga mapema ili waweze kutimiza matamanio ya wengi kwawaka ujao. 

 Mkufunzi mkuu wa michezo kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Yohana Magongo amesema sababu kubwa ya wao kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji wao kutokufanya mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu hali ambayo imewapa wakati mgumu wachezaji kuzoeana na kuwez kujenga timu bora ambayo ingeweza kuleta ushindani.

 "Changamoto kubwa sisi tuliyonayo ni kwamba chuo chetu kinaundwa na Campus tatu kwahiyo mpaka wachezaji kuja kuzoeana inachukuwa muda , lakini sasa hivi tumekuwa na vijana wengi ambao ni wageni tumeshawafahamu tunapomaliza shimuta hii tunaanza shimuta nyingine mwaka mzima nafikiri tutarudi kivingine na tutapata matokeo" alisema Magongo.

 Mashindano hayo yanazidi kushika kasi kwa kila mchezo timu zikionekana kukataa kuwa kibonde kwa wenzake wakati huo huo kwa upande wa mpira wa miguu na mpira wa pete tayari zimeshaingia hatua ya 16 bora.
Share To:

Post A Comment: