Na John Walter-Manyara

Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, Peter Toima, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara.

Msimamizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akitangaza matokeo hayo amesema, Toima ameshinda kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa huo kwa kupata kura 423 kwenye uchaguzi uliofanyika Novemba 21,2022.

Senyamule amesema Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Simon Lulu amepata kura 391 na Fratern Kwahhison ambaye hakuwa ukumbini amepata kura tatu.


Share To:

Post A Comment: