Na John Walter-Manyara 

 Nawakumbusha tu kuwa uchaguzi ndani ya chama cha Mapinduzi ngazi ya mkoa upo mbioni huku wagombea wakiwa matumbo joto kuwania nafasi hiyo kubwa katika chama. 

 Katika mkoa wa Manyara hawa ndo wagombea na pia wapo ambao wamejiandaa kupambana na Ndugu Simon Lulu anaemaliza muda wake kwenye uwenyekiti. 

 Mwenyekiti wa sasa wa Mkoa, Simon Lulu yeye anatetea nafasi yake akipambana kwenye nafasi hiyo na Balozi Philip Marmo na Peter Toima.

 Nafasi ya katibu wa itikadi na uenezi ni Mosses Komba ambaye anamaliza muda wake nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Manyara, Iddi Sulle na Johannes Darabe. 

 Mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) NEC waliochukua fomu ni Joachim Muungano ambaye anatetea nafasi yake, Dk Mary Nagu aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Hanang'kwa Miaka zaidi ya 10 hadi alipoondolewa na Mhandisi Samweli Hayyuma katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Mwingine anaegombea nafasi hiyo ni Lenganasa Soipey.

 Awali ratiba ilikuwa ikionesha kuwa Uchaguzi huo ungefanyika Novemba 2,2022 lakini umesogezwa mbele tarehe ambayo bado haijawekwa wazi.
Share To:

Post A Comment: