Serikali imetoa kiasi cha Sh44 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa kampasi tatu za vyuo vya uhasibu katika mikoa ya Arusha, Manyara na Songea.

Katika fedha hizo Sh11 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kampasi ya Arusha, Sh14 bilioni zitajenga chuo cha uhasibu Manyara na Shilingi 17 bilioni zitakamilisha ujenzi wa chuo cha Songea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dk Cairo Mwaitete wakati wa mahafali ya tatu ya shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi yaliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) kilichopo Monduli Arusha.

Amesema huo ni mpango wa Serikali wa kupeleka vyuo vya elimu ya juu katika maeneo mengine ya nchi na kwa sasa imefanya mageuzi makubwa kielimu ya kuwakomboa wanyonge.

“Rais Samia umetupatia Shilingi bilioni 44 kupitia mradi huo wananchi wote wanautazama mradi huu kama miongoni mwa miradi itakayoleta mafanikio makubwa, kukuza kipato na kuinua ajira kwa wananchi haya ni mageuzi makubwa watu wa kima cha chini watanufaika kupitia elimu,” amesema Dk Mwaitete.

Pamoja na hayo amesema mageuzi hayo yatasaidia pia kuboresha mitaala ya chuo hicho ikiwemo mitaala ya uanagenzi.

“Umetupatia fedha za maendeleo  bilioni 3, hizi zinaenda kusaidia kampasi yetu ya Manyara tunaamini maboresho haya tutaweza kudahili wanafunzi 25,000 ifikapo mwaka 2025,” amesema Dk Mwaitete.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali kazi za jeshi na kutoa kipeumbele kwa kuzingatia bajeti za ulinzi na usalama.

“Nikupongeze kwa jinsi unavyoiendesha nchi yetu, dunia nzima inapita katika misukosuko ya kiuchumi. Umetoa ruzuku kwenye mafuta, vyakula, mbolea hii yote ni jitihada za kutafuta majawabu kwenye matatizo yanayoikabili nchi,” amesema Dk Mwigulu.

Share To:

Post A Comment: