Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Eliamani Sedoyeka amesema wizara hiyo inafanya juhudi za kuwaongeza wanawake katika na sekta ya utalii, ikiwa pamoja na kuwadhamini katika masomo ya sekta hiyo.

Profesa Sedoyeka ameyasema hayo leo Novemba 26, katika Kongamano la 'Sneakers and Heels' lililoandaliwa na Chama cha Wachumi Tanzania, katika Hoteli ya Hyyat Regency jijini hapa kwa lengo la kuwawezesha mwanamke katika utalii.

Amesema kama wanawake wakiongezeka katika sekta hiyo, wataongeza tija ya kuendelea kuvutia watalii kutokana na ukarimu walionao.


"Kuhusu masuala ya utalii Tanzania kati ya asilimia 60 hadi 70 ni wanamke, lakini changamoto inaonekana kuna baadhi ya maeneo wanawake hawajaweza kufanya vizuri hususani katika eneo la kuongoza watalii, hivyo wizara imeshaanza kufanya jitihada tofauti ilikuongeza wanawake katika eneo hilo," amesema.

Kwa upande mwingine, Profesa Sedoyeka amegusia changamoto ya moto katika mlima Kilimanjaro uliotokea Oktoba 21, 2022 akisemakwa sasa moto huo umeshadhibitiwa.

"Moto ulizima kabisa wote, na bahati nzuri haukuathiri njia za utalii, kwani kwa mda wote ambao tulikua tunapambana na moto tulihakikisha maeneo yote ambapo watalii wanapita hapaathiriwa," amesema.

Kuhusu suala la kuweka uwanja wa helkopta katika mlima huo, amesema viwanja hivyo huwa mara nyingi ni kwa ajili ya masuala ya uokozi.

"Viwanja hivyo ni mahususi katika masuala ya uokozi na sio kwa ajili ya usafiri katika maeneo ya mlima," amesema.

Kwa upande wake Zuhura Muro ambaye ni mmoja wa waratibu katika taasisi ya 'Sneakers and Heela' anayewajengea uwezo wanawake katika sekta hiyo, amesema bado mchango wa wanawake ni mdogo.

"Mamlaka husika inatakiwa kuzingatia hili, kwani wanawake tunanafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika hii sekta ya utalii," amesema.


Naye mdau wa utalii, John Ulanga ambaye ni Mkurugenzi wa TradeMark Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, amesema kongamano hilo siyo kuwashika tu mikono wanawake, bali pia ni nafasi kwa wanaume kuitumia kunufaika.

Share To:

Post A Comment: