Na Denis Chambi ;TANGA.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba amewataka wananchi wanaojishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo vyakula kuyatumia mashindano ya SHIMIWI'  yanayofanyika kitaifa Mkoani hapa kama fursa ya kuweza kujiingizia kipato na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika uwanja wa Mkwakwani Mgumba amesema kuwa kufanyika kwa mashindano hayo ndani ya mkoa wa Tanga ambayo yanahusisha Wizara idara na Taasisi za ki serikali kote nchini mbali na kuimarisha afya katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ni fursa pia kujenga mahusino baina ya wafanyakazi kutoka Mikoa mbalimbali.

"Kuja kwa Watumishi wote hapa kwetu zaidi ya timu hamsini  ni uchumi mkubwa sana kwa watu wa Tanga na Taifa kwa ujumla kwa sababu  wanakaa zaidi ya siku kumi na tano wote hao wanatengeneza uchumi wa Taifa letu mashindano haya yameleta hamasa kubwa sana kwahiyo tutumie hii fursa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo za uuzaji wa vyakula, wapo wamiliki wa nyumba za kulala wageni, serikali haijakosea kuleta mashindano haya ndani ya Mkoa wa Tanga" alisema Mgumba.

Aidha Mgumba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan  kuruhusu michezo  kufanyika kwa Watumishi wa umma ambayo inaweza kulifungua Taifa kupitia sekta hiyo nje ya mipaka ya Tanzania.

"Ni Jambo kubwa na ni jema, tunamshukuru Sana Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wote wa Taasisi za umma kwa kuridhia na kuruhusu Watumishi na kuwapa vibali vya kuja kushiriki mashindano haya

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu kutoka wizara ya uwekezaji viwanda na biashara Veronica Nchango ameitaja michezo kama sehemu ya utendaji bora wa wafanyakazi wanapokuwa katika majukumu yao ya kila siku.

"Wizara yetu tumejipanga vizuri katika kushiriki kwenye michezo hii tukitambua kuwa ni afya , ni changamoto pia katika afya ya akili kwa sababu mchezaji anapocheza akili yake inakuwa  vizuri  kwahiyo na utendaji bora ofisini unaongezeka , na ukipata mfanyakazi mwenye afya  njema ndio atakufanyia kazi yako vizuri" alisema Nchango.

Mashindano hayo ambayo yameanza  kufanyika tangu October mosi yatazinduliwa rasmi kesho jumatano na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa huku yakihitimishwa October 15, 2022 yakibebwa na kauli mbiu ya Mazoezi mahala pa kazi huondoa magonjwa yasiyoambukiza . 


Share To:

Post A Comment: