BODI ya tisa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), imezinduliwa leo Oktoba 8 na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ambaye ameombwa kuidhinisha Sh bilioni 2.6, kwa ajili ya kukabiliana na upotevu wa maji yanayozalishwa.

Ombi hilo limewasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA, Mhandisi Nicas Mugisha, kwamba mpaka Oktoba 2021 waliondoa mtandao chakavu na kuweka mtandao mbadala wa maji, kilomita 9.158 kutoka kilomita 58.456 zilizokuwepo Oktoba 2018.

“Kumebakia kilomita 49.306 za mtandao chakavu wa maji, ambao imethibitika ni chanzo kikubwa cha upotevu wa maji yanayozalishwa,” alisema Mhandisi Mugisha.

Amesema kazi hiyo ilitekelezwa kwa fedha zilizotokana na mapato ya ndani, kwamba endapo kiasi kinachoombwa kitapatikana watapata bomba mpya na kuondoa mtandao chakavu uliyobakia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Halfan Haule akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee, amemshuku Waziri Aweso na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuupelekea mkoa huo fedha kwa ajili ya miradi ya maji.

“Mwaka wa fedha uliopita tulitengewa shilingi bilioni 19 ambazo tulizipata zote na zimetekeleza miradi 91 mwaka huu tumetengewa shilingi bilioni 24 kutekeleza miradi 69, lakini mpaka robo ya kwanza imekwisha, hatujapokea kiasi chochote,” amesema.

Amepongeza ubunifu wa MUWASA kwa kuingia makubaliano na Benki ya Equity, kukopesha wananchi malipo ya gharama za kuunganishiwa huduma za maji, ambazo wanazilipa kidogo kidogo

Share To:

Post A Comment: