Na,Jusline Marco:Arusha

Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Halmashauri ya Meru Bi.Aurelia Kiwale amezipongeza shule binafsi kwa kuendelea kuunga mkono serikali katika harakati za kutoa elimu iliyo bora.

Bi.Aurelia ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maafali ya 5 ya darasa la 7 katika shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kingereza ya Precious iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Ameeleza kuwa suala la kuanzisha shule binafsi lipo kisheria,ambapo pia amewapongeza wazazi na walezi kwa kuendelea kuwaamini walimu ambao wanaowafundisha watoto wao katika maadoli na misingi ya imani na hofu ya Mungu.

Ameuhimiza uongozi wa shule hiyo kuweka kipaumbele katika suala la motisha kwa walimu na wanafunzi ili kuweza wazidi kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na uwekaji wa miundombinu bora ambayo itamuwezesha mwanafunzi kujifunza katika hali ya utulivu hali ambayo itachangia ukuwaji wa taaluma.

Pamoja na hayo amewataka wanafunzi hao kufahamu pia kuhitimu elimu ya msingi siyo mwisho wa kusoma badi ni mwanzo wa safari ya elimu iliyombele yao ambapo ameshauri uongozi kushirikishwa wanafunzi katika masomo ya stadi za maisha kwa vitendo ili kuweza kutoa kizazi kilicho na ujuzi wa kimaisha.

Katika risala yake Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Debora Kileo mbele ya mgeni rasmi amesema pamoja na changamoto zinazoikabili shule hiyo, pia ina malengo mbalimbali ikiwemo uungaji mkono juhudi za serikali za kupambana na adui ujinga katika kuinua kiwango cha elimu nchini.

"Lengo lingine la shule yetu ni kusaidia na serikali kutoa ajira kwa baadhi ya wananchi ,kuwale watoto kiakili,kimwili,kiroho na kimaadili ili waweze kuwa raia na viongozi wema hapo baadae pia tuna malengo ya kuweka mikakati ya kufanya vizuri kitaaluma kuanzia kata,wilaya,mkoa na hatimaye kuwa wa kwanza kitaifa."alisema mwalimu Dabora Mkuu wa Shule ya Msingi Precious


Akito tarifa ya matokeo ya darasa la 7 kiwilaya,kimkoa na kitaifa Mwl.Debora  ambapo katika mwaka 2018 shule ilishika nafasi ya 16 kiwilaya kati ya shule 167,kimkoa nafasi ya 10 kati ya shule 293 huku kitaifa ikishika nafasi ya 106 kati ya shule 6726 kwa watahiniwa 9,mwaka 2019 shule ilishika nafasi ya 3 kati ya shule 75 kiwilaya na kimkoa ikishika nafasi ya 16 kati ya shule 322 huku kitaifa ikishika nafasi ya 157 kati ya shule 7102 kwa watahoniwa 11.

Ameongeza kuwa katika mwaka 2021 shule ilikuwa ya 1 kati ya shule 71 kiwilaya na kimkoa ikishika nafasi ya 9 kati ya shule 290 huku kitaifa ikiwa shule ya 81 kati ya shule 5664 kwa watahiniwa 37 ambapo amesema matokeo hayo yametokana na juhudi za walimu,wanafunzi na ushirikiano wa wazazi na walezi katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao.

Aliongeza kuwa shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2016 imeendelea kukua skku hadi siku kutoka wanafunzi 85 hadi kufikia wanafunzi 439 ambapo idadi hiyo imejumuisha wanafunzi wanaofadhili 70 na wanaoishi katika mazingira magumu 20.

Mzazi mwakilishi katika maafali hayo pamoja na pongezi alizozitoa kwa wakurugenzi wa shule hiyo kwa maono waliyonayo pia amewataka wahitimu hao kuendelea kuongeza bidii katika masomo yao huku wakifahamu kuwa elimu ya darasa la 7 ni msingi bora wa elimu nyingine za juu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Ndg.William Modest amewashukuru wazazi na walezi kwa kuendelea kuwaamini na kuwapa watoto wao kuwafundisha kwani hakuna kazi yoyote isiyokuwa na changamoto.

"Nawashukuru wazazi kwa kutuamini na kuwaleta watoto wenu hapa shuleni nin uhakika kwa asilimia zote watoto hawa watafaulu wote maana uwezo wao kitaaluma ni mkubwa sana."Alisema mkurugenzi huyo wa shule Ndg.William Modest

Baadhi ya picha zikionyesha matukio mbalimbali ya wahitimu wa darasa la 7 wakipokea vyeti vyao vya kuhitimu elimu ya msingi katika shule ya Msingi ya Precious iliyopo katika eneo la Nshupu Wilayani Arumeru.
Share To:

JUSLINE

Post A Comment: