Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akiongoza Kongamano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere lililofanyika wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo akizungumza katika Kongomano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere lililofanyika wilayani humo..
Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki ,Jacob Koda akichangia jambo kwenye kongamano hilo.

Kongamano likiendelea. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Thomas Abson, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maige na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Same, Abdillah Mnyambo.

Mada zikitolewa.
Kongamano likiendelea.

Mada zikiendelea kutolewa kwenye kongamano hilo.

Kongamano likiendelea 

Na Mwandishi Wetu, Same Kilimanjaro. 

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo amefungua Kongomano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere ambalo pamoja na mambo mengine limejadili maono mbalimbali ambayo baba wa taifa aliyoyafanya enzi za uhai wake.

Mpogoro wakati akifungua kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina jitihada ambazo zilifanywa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja na kudumisha mshikamano huku akipenda kuona watu wake wanapiga hatua kimaendeleo.Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki,Jacob Koda ameiomba Serikali kufufua Viwanda vyote vilivyokuwa vikifanya uzalishaji enzi za Mwalimu Nyerere ikiwa kama njia mojawapo ya kumuenzi Mwalimu.

Kwa upande wake Askofu Koda aliyasema hayo wakati akitoa mada kuhusu Mchango wa Mwalimu katika kukuza uchumi na Maendeleo endelevu ambapo alisema Nyerere alijitahidi kuanzisha viwanda katika mikoa mbalimbali ili kukuza uchumi.

Alisema Baba wa Taifa alitambua ili nchi iweze kuwa na Maendeleo endelevu lazima kuwe na viwanda na ndipo alipoanzisha viwanda vya nguo kwenye mikoa karibu yote,kulikuwepo na viwanda vya ngozi vikitengeneza viatu,mabegi,kulikuwepo na viwanda vya magunia na kiwanda Cha General Tyre cha Arusha ambacho kilikuwa kinaaaminika kwa matairi bora Afrika Mashariki.

Wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo aliahidi kuuchukua ushauri wa Askofu na kuufanyia kazi.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilitolewa na watoa mada wabobezi waliopata bahati ya kumjua Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: